Wahenga: mnamkumbuka Alexander fu sheng & Jack Chan, mapacha wa mama tofauti..

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,681
106,794
Salute..
Kwa wale vijana wa zamani, mnzikumbuka muvi za wakongwe wakali wa kung fu kutoka China. Enzi hizo miaka ya 70 Hongkong ndio kulikua Na solo LA filamu huku muvi karibia zote zikitengenezwa Na kampuni ya Shaw Brother.
images (8).jpg

Sasa bwana kulikia Na makundi mbali mbali ya waigizaji ila kundi nalozungumzia ni kundi LA akina David Chang lililotoa muvi kale kama Five masters of shaolin,Savage five,36 chamber of shaolin.

Twende kwenye mada..
Kwenye hilo kundi kuna dogo flani alikua anaitwa Alexander fu sheng, huyo jamaa alikua anafana kila kitu Na Jack chan kuanzia kuongea,vituko Na vichekesho vyao kupigana, sura hadi nywele. Bahati mbaya doho kafariki 1983 akiwa Na 28yr kwa Automobile accident. Waweza mcheki kwenye muvi kama 5 master of shaolin, savage 5, 36 chambers of shaolin: shaolin disciples. Etc huyu jamaa alinichanganya sana nilipokua Mdogo nikidhani in Jack.

Alexander
images.jpg
images (1).jpg
images (2).jpg
images (3).jpg
images (4).jpg
images (5).jpg


Jack.
images (6).jpg
d4628535e5dde711f1955e57a7efce1b9c1661cf.jpg
images (9).jpg
images (10).jpg
images (11).jpg
unnamed (1).jpg


Usisahau kua Jack alikula bata tumboni kwa mama ake muda wa miezi 12
 
Hiki kipande hua nacheka sana maana walikua marafiki kumbe mmoja yupo kwa maadui, wamekutana dogo anamfanyia comedy
Cc
Wick
 
haa mkuu labda miaka ya 50 huko ila kuanzia 70 Golden harvest presentation alikuwa anakimbiza sana mastaa wote wa kichina walioitambulisha china katika soko la firamu dunia wametolewa na Golden harvest chini ua mzee mzima RAYMOND CHOW na LEONARD HO baada kuikimbia SHAW BROTHERS kuazisha studio yao GORDELN HARVEST kuanzia mzee mzima mwenyewe BRUCE LEE alipoanza na The big boss filamu ya bajeti finyu kabisa lkn iliyofanya maajabu kabisa kiasi watu wote kumgeuzia macho mawiliwili Bruce kiasi hata mzee RAYMOND CHOW na mchizi waje HO wabaki kuduwaa
toka hapo ikawa bandika bandua 70 yote mpk 80 mpk 90 gorden harvest alikuwa anaipua vitu hatari akiwa na kina Sammo Hung jackchan yuen biao jet li nk

halafu mkuu unajua kuwa comedian hatari kabisa wa uchina ni stephen chow na mwenzie Yuen biao sema ndo hivyo hollywood iliwapotezea kwa 7bu kadha wa kadha hawajulikani sana ila hao jamaa ukicheck movie zao huchoki kuburudika mfano hutaburudika
bila kumsahau sammo hung comedian kibonge anayevunja mbavu ukibonge wake unaburudisha hasa enzi hizo akicheza na Ka Yan Leung utaburudika kwa comedy za kiwango cha juu

kwa ufupi movie za kichina za zamani ni nzuri sichoki kudownload
coz km ni mkono unakuwa ule halisi sio sasa computer nyingi hasa ukute movie ya ANCIET CHINA zile za kijijini naburudika sana mababu wale na midevu yao meupe wanapiga karate ile ile hasa wakikutana milimani huko kila mtu anaonesha stail yake halisi kabisa Kama mfano INVINCBLE ARMOUR hii inaonyesha jinsi unaweza tengeneza mwili na usiingie hata kisu ndani ya hii movie yumo Yuen biao na COREY YUEN(kama unaijua movie ya EAsten condors basi kacheza anavuta sana sigara mpk anakufa darajani huku fegi mdomoni)

7 GRANDMASTER hao maticha kila mtu ana stail yake sasa huo mkono wa humo hatarii
zipo movie nyingi zinapiga karate halisi kabisa kiasi ukiangalia burudani tosha

bila kusahau movie zao za Romantic comedy drama kama zile mfulilizo wa CHINESE TORTURE CHAMBER STORY au SEX AND ZEN humo utakutana na wakari wa romantic comedy kina ELVIS TSUI na schoral LAWRENCE NG
bira kusahau hii movie ya
THE FORBIDDEN LEGEND SEX AND CHOPSITCKS sema hii ya miaka 2000 ile imechezwa vema kabisa kama vile
pia kuna The Golden Lotus ya 1974 kwenye hii movie yupo jack chan lakini huwez mjua km yeye pia yumo DEAN SHEK (huyu unamjua vizuri sana kacheza movie nyingi na jack chan kijamaa chembamba kina mikwara lkn kupigana hajui ila usimfananishe na
PAUL WEI PING AO naye stail zake km huyu kacheza zaidi na BRUCE kwenye the way of dragon akiwalazimisha wauze hoter yao bruce anawapa kipondo mpk jamaa na boss wake wanamleta CHUCK NORIS kumdhibiti bruce na FIRST OF FURY mchina anaejipendekeza kwa wajapani na mikogo mingi inayovutia sema jamaa kavuta tangu 1989)
pia kuna mfulizo wa
EROTIC GHOST story
mfululizo wa BROTHER OF DARKNESS humo utamkuta kichaa comedy wa staili za kibabe na na kufosi KA KUI HO sema jamaa nae kashakufa mwaka juzi na nyingne nyingi tuu


movie za china za zamani zilikuwa nzuri sana
 

Attachments

  • stephen chow.jpeg
    stephen chow.jpeg
    16.7 KB · Views: 37
  • Ka Yan Leung.jpeg
    Ka Yan Leung.jpeg
    10 KB · Views: 34
  • DEAN SHEK.jpeg
    DEAN SHEK.jpeg
    11 KB · Views: 33
  • Paul Wei Ping-ao.jpeg
    Paul Wei Ping-ao.jpeg
    12.7 KB · Views: 38
  • ELVIS TSUI.jpeg
    ELVIS TSUI.jpeg
    10.8 KB · Views: 34
  • ELVIS TSUI 2.jpeg
    ELVIS TSUI 2.jpeg
    12.4 KB · Views: 33
  • COREY YUEN.jpeg
    COREY YUEN.jpeg
    17.2 KB · Views: 45
  • Ka Yan Leung6).jpeg
    Ka Yan Leung6).jpeg
    5.6 KB · Views: 39
  • Ka Yan Leung na yuen biao.jpeg
    Ka Yan Leung na yuen biao.jpeg
    20.7 KB · Views: 35
  • Ka-Kui Ho.jpeg
    Ka-Kui Ho.jpeg
    13.7 KB · Views: 46
  • Ka-Kui Ho 1.jpeg
    Ka-Kui Ho 1.jpeg
    9.9 KB · Views: 42
  • stephen chow.jpg
    stephen chow.jpg
    36.8 KB · Views: 42
  • Yuen biao.jpeg
    Yuen biao.jpeg
    14.5 KB · Views: 36
  • yuen biao sammo hung chung fat na Ka Yan Leung.jpeg
    yuen biao sammo hung chung fat na Ka Yan Leung.jpeg
    39.8 KB · Views: 49
  • kent cheng 1.jpeg
    kent cheng 1.jpeg
    19.9 KB · Views: 36
  • kent cheng.jpeg
    kent cheng.jpeg
    7.8 KB · Views: 38
  • Shun-Yee Yuen.jpg
    Shun-Yee Yuen.jpg
    43.9 KB · Views: 26
  • Shun-Yee Yuen.gif
    Shun-Yee Yuen.gif
    3.3 MB · Views: 36
  • richardng.jpg
    richardng.jpg
    8 KB · Views: 40
haa mkuu labda miaka ya 50 huko ila kuanzia 70 Golden harvest presentation alikuwa anakimbiza sana
hila movie za kichina za zamani ni nzuri sichoki kudownload
coz km ni mkono unakuwa ule halisi sio sasa computer nyingi hasa ukute movie ya kijijini naburudika sana mababu wale midevu ya meupe wanapiga karate ile ile
Nimeona muvi nyingi sana za kichini sana.
No kweli Raymond Chow alikuja kubadiri gemu LA muvi za kichina baada ya kuanzisha kampuni ya Golden Harvest, pia usimsahau Director na producer bora Yuen woo ping
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom