Wahariri mmenishangaza sana

Wahariri mmenishangaza sana

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,178
Reaction score
162,654
Leo nimesikiliza kipindi cha magazeti kupitia Channel 10 lakini nimeshangazwa sana na kitu kimoja.

Kama mnavyofahamu,Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu hapa nchini,jana walitoa tamko kupinga katiba kwa kigezo cha mahakama ya kadhi kutokuwepo katika katiba inayopendekezwa.

Binafsi, sikubaliana na msimamo wa jumui hizo lakini kinachonishangaza ni kuona habari hii imepewa kisogo na magazeti mengi isipokuwa matatu ambayo ni Tanzania Daima,Jambo Leo na The Guardian tu.Mwananchi halikusomwa.

Yaani hii habari kwa wahariri wengi kwao si habari!Magazeti ya serikali ndio kabisa yote yamekwepa kuripoti habari hii.

Nilitarajia hii habari kama sio kuwa habari kuu,basi ingepewa walau hata uzito mdogo lakini hali imekuwa tofauti kabisa utadhani hili ni jambo dogo sana lisilo na athari yoyote kwa taifa hili.

Hivi hii tamko si jambo zito kwa upande wa katiba inayopendekezwa?Mnangoja waanze kujadili misikitini ndio mripoti?

Waandishi, kuficha vitu vingine ni kujidanganya tu kwani vinagusa umma moja kwa moja na vina impact kubwa sana.Leo mtaficha hii habari lakini ni nyinyi hao hao ambao kesho na keshokutwa mtakuja kuripoti yatokanayo na tamko hilo na hapo sijui mtakuwa mmekwepa nini?

Hatua hii ni sawa na kujaribu kuficha moto wakati moshi unafuka.Uamuzi wenu hauisadii serikali wala umma bali ni kujidanganya tu.Timizeni wajibu wenu.
 
Wahariri wengi wapo kimaslahi na wala si kuhudumia jamii.
 
Salary Slip nakuhakikishia hiyo ina impakti kubwa mno. Wai acha wafiche Kilama misikitini kupitia sala za ijumaa mbivu na mbichi itajulikana.
Katiba pendekezwa misikitini ni lazima itaingelewa na si kwa uzuri bali waislamu kuhamasishana na kuipigia kura ya hapana.
Ngoja tuvisubiri hivyo vyombo vya habari ambavyo haviko tayari kutoa taarifa iliyosomwa mbele yao waje WASEME WAISLAMU WANAFANYA SIASA MISIKITINI.
 
Tamko halina maana that is why waharir wamelipa kisogo
Huku ni kujidanganya mchana kweupe!

Hawa jamaa wakikomaa hili jambo litakuwa na impact kubwa kwa taifa hili na hapo kutakuwa hakuna kukwepa tena bali watakuja kuandika hiyo habari na pengine wakilaani matokeo yake.

Sasa hapo watakuwa wamemsaidia nani na watakuwa wamefanya nini?
 
Huo nao ni mpango wa Mungu!!!!
 
Pole for having high expectations on our local media... they are extremely poor ... nipeni gazeti moja ambalo unaweza ulisome alafu urudie kulisoma tena.
 
Salary Slip nakuhakikishia hiyo ina impakti kubwa mno. Wai acha wafiche Kilama misikitini kupitia sala za ijumaa mbivu na mbichi itajulikana.
Katiba pendekezwa misikitini ni lazima itaingelewa na si kwa uzuri bali waislamu kuhamasishana na kuipigia kura ya hapana.
Ngoja tuvisubiri hivyo vyombo vya habari ambavyo haviko tayari kutoa taarifa iliyosomwa mbele yao waje WASEME WAISLAMU WANAFANYA SIASA MISIKITINI.

Jana nimeswali Magomeni swala ya ijumaa,baada ya swala ukafuata uchambuzi wa mahakama ya Kadhi na katiba pendekezwa na mwisho ikashauriwa kupiga kura ya Hapana.
 
Pole for having high expectations on our local media... they are extremely poor ... nipeni gazeti moja ambalo unaweza ulisome alafu urudie kulisoma tena.

Zamani ilikuwa ----------- na Raiamwema, ----------- akapigwa ban akabaki Raiamwema ya kina Generali Ulimwengu lakini siku hizi na yenyewe hakuna kitu kabisa. Labda the Citizen.
 
Jana nimeswali Magomeni swala ya ijumaa,baada ya swala ukafuata uchambuzi wa mahakama ya Kadhi na katiba pendekezwa na mwisho ikashauriwa kupiga kura ya Hapana.

Habari hizi wao kwa ndio habari.Wanapenda kuripoti matokeo na si chanzo chake.
 
Back
Top Bottom