bwanafundi
Member
- Jan 13, 2011
- 17
- 1
wanajukwaa naomba tujadili juu ya athari ya vita ya uganda maana waliokuwa vijana wakati vita vinapiganwa kati ya nchi yetu na idi amini wa uganda waliozaliwa mwaka 1955 hadi 1975 kwa kweli mtaji wao wa nguvukazi ulitumika kwa maslahi ya watawala,na ni ukweli ulio wazi kuwa ujanawao wameumalizia kwenye miezi 18 ya dhiki na kupewa asante ya maneno tupu na mtawala na hapa ikumbukwe na izingatiwe kuwa sizungumzii wanajeshi ila vijana wakulima ambao walikosa vitu vyote muhimu ambapo kuvikosa ni kukosa ile maana halisi ya maisha bora,haya hivi karibuni tu ndio kumepambazuka kiuchumi na wao tayari ni wazee wameshapitwa na utafutaji wa maisha,na kwa taarifa yenu hilo kundi ndilo fukara zaidi hapa tanzania tena wengi wao ni walevi.nawaomba tusaidiane watu wetu hawa walipwe fidia wakati huu wa neema kwa taifa letu maana jasho lao ndilo lilifanya taifa letu limshinde idi amini, na kujifanya hatujui shida waliyopata wazee hawa ni dhambi tena laana kwa taifa lote la tanzania.