Wahandisi tunataka kila anayejenga ghorofa lazima usanifu na ujenzi atumie wahandisi

Kumbe mna bei nafuu hivo...mbna hamsemi....watu wanaogopa gharama zenu
 
Ninawafaham mafundi wa mitaani waliochora na kujenga nyumba vizuri zaidi kuliko hao mainjinia wenu. Elimu ya kwenye daftari na ya field ni vitu viwili tofauti.
 
Kwani Sheria zinasemaje?

Wewe Mhandisi alafu haujui Sheria?, Ramani mpaka ipitishwe na mipango miji n.k. lazima structure engineer awe amefanya kazi yake.., sasa kwa kutokupitisha huko au mtu kupiga muhuri kabla ya kufuata vigezo vyote (soil test n.k.) sio mapungufu ya Sheria bali utekelezaji...

Na kama bei zinazowekwa sio rafiki unategemea nini kama watu sio ku-cut corners....

Ni mambo mengi hata wiring / electrical installations mwisho wa siku zitakuwa zinafanywa na certified electrician ambaye kila mwaka anatakiwa kufanya checjk-up..., bila kufanya hivyo hata kama una Bima unaweza kujikuta Ukipatwa tatizo haulipwi sababu umekiuka vigezo

Anyway huko ni mbali sana kufika ukizingatia kipato cha walengwa ni cha kubangaiza kwahio sheria haziwezi kuwa strictly sana
 
Wewe Mhandisi ili nikuamini unaweza wewe umefanya nini cha kihandisi ukiondoa ile project uliyopewa na instructor wako aka propesa
 
Na akija Mhandisi kwangu lazima na mwanasheria awepo, tusainishane mkataba wa kazi na ikiharibika uweze kulipa gharama zote
 
Hao walitaka kumuibia fundi
 
Wewe Mhandisi ili nikuamini unaweza wewe umefanya nini cha kihandisi ukiondoa ile project uliyopewa na instructor wako aka propesa
Wahandisi wana board inayowasimamia inaitwa ERB( engineer registration board) ili usajiliwe lazma wamethibitisha capability yako ya ufanyaji kazi pamoja na kaz ulizozifanya kwahio ili mtu aitwe mhandisi be lazma amethibitiswa na board na anaruhusiwa kufanya shuhuli za kiuhandisi . Ukihitimu tu chuo na degree yako bado hujawa mhandisi mpaka board itakapo kusajili
 
kwa yaliyotokea DSM ni msisitizo kuwa tunahitaji kuweka wataalamu katika ujenzi na wao wawajibike kama makosa yakitokea ingawa tunatambua kuwa makosa mengi yanafanyika kwa sababu ya kukosa uelewa na lengo la kuingiza wataalamu kama hitaji la kisheria ni kusaidia jamii kupunguza madhara, kupunguza gharama na kuongeza ubora.
 
Wazo zuri sana...lakini ushauri wang kwa wahandisi waweke gharama ambazo ni nafuu sana ili kuweka mazingira rafiki kwa hawa clients.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…