Wahamiaji wavamia Mvomero kusaka dhahabu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Wahamiaji wavamia Mvomero kusaka dhahabu
Mwandishi Wetu, Mvomero
Daily News; Monday,July 28, 2008 @20:13

Raia wa kigeni wameingia kwa wingi kinyemela katika milima ya vijiji vya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kwa lengo la kutafuta madini ya aina mbalimbali yakiwamo ya dhahabu bila kupata idhini na utaratibu wa kisheria wa mamlaka ya viongozi wa serikali ya wilaya.

Kutokana na wimbi hilo la wageni kuingia kinyemela hasa raia wa Korea katika maeneo ya vijijini, Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Hawa Ngh’umbi, ameziagiza mamlaka za serikali za vijiji na wananchi kwa ujumla kuwafichua wageni hao katika vyombo vya dola.

Wilaya ya Mvomero katika Kata ya Maskati na Kibati Tarafa ya Mvomero ni miongoni mwa maeneo yanayosadikiwa kuwa na madini ya aina mbalimbali yakiwamo ya dhahabu na uchimbaji wake hufanyika kando kando ya kingo za mito na ndani ya mito.

Ngh’umbi alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wakati akifungua kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mvomero na alipozungumza na wananchi wa Kata ya Maskati wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Saidi Kalembo.

“Wapo watu wanaingia katika maeno mbalimbali ya kata za wilaya yetu bila ya kutoa taarifa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hasa wageni wa kutoka mataifa ya nje…Juzi walikutwa wa raia wa Korea wakiwa milimani katika Kijiji cha Kinda na hawakuwa na barua ya kupitia ofisini kwangu,” alisema DC Ngh’umbi.

Alisema mbali ya raia kukutwa na msafara wake katika siku hizo, pia kulithibitishwa na Diwani wa Kata ya Maskati, Romanus Mhando, kuwa raia wao walivamia milima ya Kijiji cha Kinda wakiwa na lengo la kufanya utafiti wa maeneo yatakayoweza kupatikana kwa madini.

“Wakorea hawa nimewakuta juzi njiani, lakini pia amenithibitishia Diwani wa Kata ya Maskati kuwa Wakorea hao wameweza kupanda katika milima ya Kinda na waliingia eneo hili bila ya kuwa na barua ya ofisi yangu,” alisema. Aliwataka wananchi kutowapokea wageni kutoka nje ya nchi wanaoingia kinyemela katika vijiji, ambao hawafahamiki kwa kuwa dunia ya sasa imetawaliwa na vurugu na machafuko, hivyo kuwapo wao ndani ya maeneo ya vijiji hivyo kunaweza kuleta hatari kwa taifa.
 
Back
Top Bottom