Nikiongezea kwa jibu la ndg. min -me sio ajira pekee bali pia ni sababu za kiuchumi na ubinafsi zinachangia.
Tukiangalia orodha mbalimbali za watia nia wengine ni wafanyabiashara wakubwa sana hapa Tanzania, wengine ni maprofesa, wengine ni wastaafu serikalini, ubunge, Uspika wa Bunge, Uwaziri nk. ambao walikuwa na nyadhifa za juu sana, wengine katika jamii wana ukwasi wa fedha ambazo watatumia kwa miaka mingi na watoto wao mpaka wajukuu.