Wagombea hawajui maana ya Kampeni? Au ni Wananchi wasiojua maana ya Kampeni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea hawajui maana ya Kampeni? Au ni Wananchi wasiojua maana ya Kampeni?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pax, Aug 22, 2010.

 1. P

  Pax JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nilifuatilia ufunguzi wa kampeni wa chama tawala jana pale jangwani na kwa kweli nilisikitika nilichokuwa nasikiliza. Wote waliozungumza hawakuongea jambo la msingi la kuwashawishi wananchi wawachague, ni mashairi na ngonjera tu. Makamba anazungumzia ati wana wabunge 10 tayari, so what? Dr. Bilali anawashukuru wenzie kumteua, so what? Raisi Kikwete anazungumzia walichofanya, mara TUKTA, mara tumepeleka watu mashuhuri mahakamani etc so what? Je hii niishara ya kuonyesha umbumbumbu tulio nao wananchi wa TZ? Umaskini wa kipato ndio umepelekea sisi wananchi kuwa na umasikini wa kufikiri?

  Kampeni ni kuwaelezea wananchi utakayowafanyia na namna utakavyotekeleza, that simpo. Sio kupoteza mda kueleza yaliyopita ambayo hayana nafasi kwenye maisha yajayo. Eleza utakavyokusanya kodi, eleza vipaumbele vyako, eleza utakavyoboresha huduma za afya, eleza utakavyokomesha rushwa, eleza utakavyokuza uchumi wa nchi kwanjia unazojua wewe, eleza elimu utafanya nini n.k. Kumpeleka mtu mahakamani sio achievement, haiwezi kukufanya wewe uchaguliwe kutuongoza. Nawashauri wagombea wengine watueleze watakayofanya na namna watakavyotimiza hayo wanayokusudia kufanya, hatuna muda wa kusikiliza porojo zisizo na mantiki.
   
 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,315
  Trophy Points: 280
  Mkuu upo sahihi kabisa!
  LAKINI jambo moja ni dhahiri.... give the people what they want!!!! Viongozi wanafanya hivyo kwa kuwa Watanzania hawamchagui kiongozi/Chama kwa sababu ya sera zake au uchapakazi wake. Wanafuata ushabiki tu.....
  Na Kikwete/CCM wanalijua hili fika. Ndio maana wanatumia uhamasishaji kwa njia mbalimbali... musiki, ngoma, ngonjera n.k. Hili linawafaa zaidi kwani hizi ndio njia za kuvutia mashabiki.
  Anyway... Ku-exercise demokrasia kwenye sehemu yenye ujinga na umaskini wa kiwango cha Tanzania ni nearly impossible mision.
   
 3. P

  Pax JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Dawa ni moja tu, kuwa na weighted votes ambazo zita consider ubora wa kura na sio idadi peke yake. Utaona kimbembe chake. Miziki, Ngonjerana kila aina ya vibwagizo zitakoma :confused2:
   
 4. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nashangaa pilipili usiyoila yakuwashia nini?Nyie fuatilieni yenu na ya CCM waachieni wenyewe!Mnajifanya mpo Chadema kumbe kila jioni mnaonekana zone za kata kupanga mikakati ya ushindi wa CCM,tunawajua nyie ni bootrickers!
   
Loading...