Wageni Wenye Nyadhifa Kubwa Dhidi Ya Athari Mtambuka kwa Taifa

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,169
1,073
Ebu tujiulize kwa nini nchi yetu ni maskini?Kwa nini mambo mengi ya ovyo yenye kuligharimu taifa yamekuwa yakifanyika pasipo kukemewa kwa kipindi kirefu?Kwa nini Mikataba ya kinyonjaji inayolitafuna taifa kila iitwapo leo?Kwa nini watendaji waandamizi walio wengi wana mapungufu ya uzalendo dhidi ya maslahi ya taifa?Kwa nini nchi yetu imekuwa shamba la bibi?Kwa nini tunabezwa hususani na baadhi ya nchi jirani?

Ni ukweli ambao wengi wetu tumekuwa tukiufumbia macho na kuona aibu kuudodosa..
Nchi yetu imejaa watu wakarimu,wapole,wanyenyekevu na wenye wingi wa upole kwa wageni wanaopita au kuweka makazi ya kudumu.Tabia asili za watanzania zimewafanya wageni wabweteke na kujiinua hata kufikia hatua ya kujiona wana haki zaidi kuliko wenye nchi yao {kisiasa,kiuchumi,kijamii,kiutamaduni}..Sisemi haya kwa ubaguzi,chuki bali

Naliona tatizo kubwa kisiasa-wageni kujipenyeza na kuwa wajasiri kufanya yasioweza kufanywa na wenye nchi...,kijamii,kiusalama-kuhujumu mipango,mikakati mahsusi na kiuchumi-kudumaza maono kwa ushauri potofu/mikataba nyonyaji......... kutokana na udhaifu wa mfumo udhibiti dhidi ya wageni toka katika mataifa ya nje na hususani mataifa jirani yenye mjamiiano wa kijiografia na kijamii kupitia makabila yenye vitako maeneo ya mipakani na taifa letu kwa kimipaka .

Mbinu nyingi zimekuwa zikifanywa na koo,familia,nchi adui kupenyeza raia wake kwa makusudi maalumu ya kimkakati {muda mrefu,muda mfupi kutegemea malengo} mfano,Kusomesha watoto ktk nchi lengwa {elimu ya awali mpaka ya juu-kusomea taaluma za utawala,uchunguzi,ICT,n.k};Kupenyeza uzao kwa kuoa au kuolewa ktk kaya kuu,kaya zenye maono,kaya tawala,Kaya zenye ukwasi n.k.;Kununua ajira ktk taasisi nyeti,taasisi mama ktk kuajiri ili kuwa daraja la ajira kwa wengine-jamaa,ndugu {mfano:Utumishi,tume ya ajira}.

Mfano udhaifu wa wenye mamlaka katika nafsi/mioyo dhidi ya tamaa za ngono toka kwa warembo/walimbwende/wanawake na wanaume wenye mvuto wa sura,maumbile,mwonekano vimekuwa vikitumiwa kama mtego/silaha kufanikisha malengo ya muda mrefu na mfupi....viongozi kuweni makini..

Tatizo lipo kwa kuzingatia uadui ,husuda,chuki,faraka zenye kusababishwa na historia ndefu na fupi kabla na baada ya ukoloni zilizojengwa kupitia mifumo ya kisiasa,kikabila,kikanda n.k. Nchi yetu inapakana na Malawi,Zambia,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Rwanda,Burundi,Uganda,Kenya,Visiwa vya Comorro,Msumbiji.

Wapo wageni wengi wenye nyadhifa za chini,za kati na kubwa {andamizi} katika taasisi za kiserikali,Mashirika ya Umma,binafsi,Vyama vya siasa na vyombo vya usimamizi wa haki,amani,usalama n.k. {Wapo wataotaka ushahidi}.Wapo wageni waliolowea hivyo kutokuwa na mizizi au matawi toka ktk nchi zao za asili ,Lakini wapo wageni wenye nyadhifa ambao bado wana mizizi ya utaifa,uzalendo,usiri,koo,familia katika nchi zao za asili.Ebu jiulize kwa nini nchi yetu ni maskini?

Kwa hawa wenye mizizi bado na mataifa yao ya asili NI HATARI SANA KWANI WAWEZA KUTUMWA NA KUWA WATII KUTIMIZA MALENGO YA WATAWALA WASIO NA NIA NJEMA NA TAIFA LETU na wakiwa na nyadhifa kubwa nchini kwetu WAWEZA ZITUMIA NYADHIFA HUSIKA KWA FAIDA YA MATAIFA YAO YA ASILI NA SI TAIFA WALILOPO{katika taasisi nyeti} tutegemee nini ? siri za nchi kuvujishwa ,mikakati makini/endelevu kuhujumiwa,utendaji makini kubezwa,ufifishaji wa makusudi wa maendeleo,Hujuma,hujuma,udumazaji wa maendeleo,Matendo yasio ya kizalendo,Ufisadi usio na huruma..

USHAURI:

MIFUMO YA UTEUZI ,UAJIRI IMURIKWE KIZALENDO ZAIDI KWA MASLAHI YA NCHI NA TAIFA.

WAFANYAKAZI WAANDAMIZI,WATENDAJI NA VIONGOZI WAANDAMIZI HASA KUTOKA MIKOA YA PEMBEZONI MWA NCHI WACHUNGUZWE/WAMULIKWE/WATAZAMWE UPYA KUBAINI UTAIFA WAO,UZALENDO WAO,...

WALE WOTE WATAKAOBAINIKA KUWA NDUMILA KUWILI /KUTOKUWA WAZALENDO/WAHUJUMU TAIFA WADHIBITIWE NA KUCHUKULIWA HATUA MAHSUSI.
 
Umeandika kwa usahihi sana, haya yote ni taadhari tuliyoitoa wakati wa kuifufua jumuiya ya AM. Kwamba katika nchi zote Tanzania ikiwa nyuma ya Uganda iliacha mianya mingi kwa wasio raia wazawa kujipenyeza kwenye mfumo wa maeneo nyeti.

Kuanzia ngazi ya mtaa hadi serikali kuu. Mfn hai ni uteuzi uliotenguliwa wa NSSF DG, hivi viashiria kwamba kila mahali watu hawa majirani wenye husuda wamepenya sana na wanaitamani TZ kwa manufaa ya nchi zao za kiasili.

Kuna kazi kubwa sana kupangua uozo huu. Na hata hapa JF utaona kuna wapingaji wengi sana wa serikali na ukiwachunguza Unakuta wengine si raia wazawa wa nchi hii.
 
Kila mtanzania mzalendo na wajibu wa kulifanyia kazi hili..madhara ni makubwa sana mbeleni,mataifa yalioendelea yana mfumo makini sana ktk kudhibiti hujuma mtandao zinazotokana majukumu/utendakazi/wajibu wa wageni kisiasa,kijamii,kiuchumi...Mfano:Tatizo la sarafu yetu kuporomoka-Tujiulize washauri wa gavana wa benki kuu yetu wanashauri ipasavyo?,Ni watanzania kweli?wana uzalendo? Ushauri wao una mashiko ktk kufufua uchumi kwa dhati?...Vipi kuhusu Elimu yetu ..TEA,NACTE,NECTA,etc....
 
Sina tatizo wala watanzania hatuna tatizo na wanaoishi kwa kufuata sheria za nchi na matakwa ya kikatiba..sina tatizo na wanaoishi kwa ustaarabu na unyoofu wa mioyo au dhamira..sina tatizo na waliokimbilia Tanzania toka ktk mataifa yao sababu ya vita,ukandamizaji,uonevu,ukabila kisha kuishi nchini kwa adabu/heshima/uadirifu/...

Wapo tele serikalini,wapo tele kwenye mashirika ya umma,Wamejaa kwenye NGO's,Wengine wanajiita wanaharakati,Makampuni binafsi,Taasisi za Fedha..Wengi wanafaidi huduma/haki sawasawa na watanzania ..Wengi wao hutumia fedha nyingi kupata passport za Tanzania,kupata vyeti vya kuzaliwa ,Vitambulisho vya uraia,Kupiga kura,wanashiriki ktk michakato lukuki kama watanzania zikiwemo biashara,wananunua mashamba ,viwanja,majumba,wanamiriki vitega uchumi ,Baadhi walijitahidi sana kuchochea nchi kuingia kwenye machafuko kabla na baada ya uchaguzi {kupitia social media}..

Si lengo langu kuchochea chuki wala ubaguzi baina ya jamii zinazoishi Tanzania...lengo ni kuhamasisha uzalendo uliotukuka ktk wajibu wa kila mwananchi kushiriki kuilinda ,kuitetea,kukemea uovu,kuhubiri haki,kweli na uwazi..Nchi yetu ilipaswa kuwa mbali sana kimaendeleo ...tupo tulipo sababu ya ndugu,jamaa au wachache tuliowapa dhamana ya kutuongoza kugeuza maslahi mapana ya taifa kuwa maslahi ya familia zao,ndugu zao,rafiki zao,makabila yao,dini zao,mataifa yao ya asili,....
 
Back
Top Bottom