Nenda sokoni kaombe matenga makubwa kwa wauza kuku (jieleze kiume hata kama ni KE - watakuazima au kukukodisha kwa bei ndogo), weka kuku kwenye tenga - katafute lori zinazorudi Dar zikiwa hazina mizigo, waombe - watakubebea kwa bei ndogo tu ukawauze Dar, utapata faida kidogo kuliko hivyo unavyowagawa bure. Changamoto za biashara kama hizo ndio zinazotofautisha vipato baadae, unayekata tamaa utaporomoka na atayekomaa atasogea.