Wafanyakazi walitaka hiki tu, mheshimiwa rais!

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,781
6,065
Kwanza nikupongeze rais wangu Magufuli kwa nia njema uliyonayo nikinukuu kauli yako uliyosema
wewe ulikuwa mwalimu na huwezi kusahau hilo. Ukasema wengine wanaweza kusahau (na pengine wameshasahau) lakini WEWE huwezi kusahau watumishi wa umma!!

Pamoja na mengi mazuri siku ile ya Mei Mosi niseme kuwa ule umati mkubwa wa watu ulimaanisha mambo mawili

1. Maisha ni magumu mno kwa wafanyakazi na walitegemea unakuja na neno moja tu la UZIMA la kuwafariji.

2. Wafanyakazi wamekuwa wavumilivu sana baada ya pilika zote za uhakiki, kusimamishwa kwa maslahi yao n.k, siku ile ya mei mosi walikuja pale wakijua the storm is over na wanaenda kucheka...

Nikirudi kwenye mada sasa pamoja na mambo mengi mazuri uliyosema lakini wafanyakzi walikuwa wanataka kusikia hiki tu...
1. Kule Zanzibar waliongezewa 100% na imekuwa hivyo kuanzia mwezi April.
2. Kule Kenya wamepata 18%

Wafanyakazi walitaka kusikia na wewe utatoa asilimia ngapi? Bi
nafsi kwa muonekano wako siku ile na ulivyoanza kuongea nikajua sasa 150% inahusika!!!

Nakumbuka mwaka jana kodi iliposhushwa kutoka 11-09 wapo watu walishangilia na kupiga vigelegele... lakini wakaja watu ambao wanajua hesabu wakasema imeongezeka 2800-3000 hivi wakatukanwa sana.

Ilipofika mwezi wa saba wote tukajionea (sitaki kukumbuka ile siku)

Ni kweli Mheshimiwa umetangaza nyongeza binafsi nina maswali kadhaa na naomba ufafanuzi kwa yeyote

1. Rais anaposema ile nyongeza "ya kawaida ya mwaka" anamaanisha kiasi gani au asilimia ngapi?

2. Nyongeza hii ilikuwa itolewe mwaka 2016-2017, sasa leo Raisi anaposema itatolewa kwenye bajeti ijayo hii nyongeza ya tangu mwezi wa saba mwaka 2016 hadi juni 2017 itakuwa imeenda wapi?
 
Aliongelea increment ya mshahara bila kutaja %. Ni sawa mtu anakuhaidi nitakupa pesa..sawa.Je akikupa 50 tsh utahamaki(huna haki ya kuuliza).Hii ndo siasa bwana.

Eti mi sio mwanasiasa.....my foot..

"Msema kweli mpenzi wa mungu"
 
Zanzibar hawajaongeza100% kwa watu wote msipotoshe umma, 100% inayoongezwa ni kwa mishahara ya kima cha chini, kwa mfano kama kima cha chini kilikua laki moja sasa kitakua laki mbili, sio kwamba kama ulikua unapokea milioni moja basi utapokea milioni mbili never.

Annual increments za miaka ya nyuma ndizo zinaweza kutupatia picha halisi ya increment tarajiwa maana hazina tofauti, wadau watatuambia hapa
 
Julai ndio ama wacheke au walie....ila ni bora kujiandaa kulia.
 
Kiukweli naweza sema waliowengi hawakuelewa.Ongezeko la mwaka kwa kima cha chini halifiki 20000,walipaswa kulipa fedha zote za ongezeko kuanzia July 2016 lakini kasema hizo fedha zitaajiri wengine. Akauliza hamutaki wenzenu waajiriwe? Wakajibu .Hapana. Hivyo ndg mwl usitarajie kisichokuwepo.
 
Back
Top Bottom