Wafanyakazi hewa sasa wako 8,236

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
SIKU chache baada ya Rais John Magufuli kutaja idadi ya watumishi hewa kuwa ni 7,200, msako unaoendelea katika utumishi wa umma, umetoa takwimu mpya ambapo sasa watumishi hao wamefikia 8,236.

Katika hatua nyingine, wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ambao wamefunguliwa kesi mahakamani kutokana na ubadhirifu, ambao wamekuwa wanatumia magari na mafuta ya umma na kujilipa posho wanapokwenda kwenye kesi zao, wataanza kuchukuliwa hatua kali.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, amesema hayo bungeni jana wakati akihitimisha hotuba yake ya bajeti kwa mwaka ujao wa fedha.

Akizungumzia wafanyakazi hewa, Waziri Kairuki alisema kati ya Machi Mosi na Aprili 24, mwaka huu, Serikali imebaini kuwepo kwa watumishi hewa 8,236, idadi inayoonesha kuwepo kwa ongezeko kubwa baada ya hivi karibuni Rais kuripoti kuwepo wafanyakazi hewa 7,200.

Alisema katika idadi hiyo, wafanyakazi hewa 1,614 wameripotiwa kutoka Serikali Kuu huku wengine 6,622 wakiripotiwa kutoka Serikali za Mitaa, na kufanya ongezeko lao kufikia 2,737.

Kwa mujibu wa Waziri Kairuki, kuwepo kwa wafanyakazi hao hewa katika utumishi wa umma kumeisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 15.4, ambazo zingeweza kutumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema katika kushughulikia hilo, Serikali imelazimika kuwasimamisha kazi maofisa utumishi 56 ambao walibainika kuhusika kufanikisha malipo ya mishahara kwa watumishi hao hewa na hatua mbalimbali za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao.

‘’Hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yao na endapo watabainika kuwa na makosa kisheria, watalazimika kurejesha fedha za Serikali zilizopotea kutokana na malipo hayo hewa ya mishahara,” alisema Kairuki.

Kuhusu wakurugenzi wa halmashauri wenye kesi za ubadhirifu mahakamani, Waziri Kairuki alisema Serikali inafanya uchunguzi kuhusu wakurugenzi hao ambao kutokana na kuwa na kesi mahakamani, wanatumia fedha na rasilimali za Serikali kwenda kuhudhuria kesi zao.

“Zipo taarifa hizo kwamba wakurugenzi hawa wanakwenda katika kesi hizo wakiwa wamejilipa posho za kujikimu za Serikali wao na madereva wao lakini pia wakitumia magari na mafuta ya Serikali. Ikibainika kuwa wapo wakurugenzi kama hawa hatua kali zitachukuliwa kwao mara moja,” alisema Waziri Kairuki.
 
Hatua nzuri
 
Hizo ela zilikua zinasaidia chama hakuna mtu aliekua anakula waache sanaaa
 
Kwa maana hiyo Serikali kwa sasa ina uwezo wa kutoa ajira zaidi ya 8000, kwasababu bajeti yao ipo ndio maana ililiwa hiyo mishahara
 
Kazi hewa - mishahara hewa. Sasa unataka Serikali iajiri wafanyakazi wafanye kazi gani, hewa?
 
Maana yangu ni kwamba hadi hao wamekuwa hewa ina maana fedha ya kuwalipa ilikuwepo, kama fedha ipo Serikali iajiri sehemu zenye upungufu wa watumishi
 
Kuna dhana ya kufanya kazi bila kulipwa ingawa aliyefanya kazi alistahili kulipwa. Hapa unaweza kusema kuwa pesa ipo, kwa maana ilipangwa kulipwa haikulipwa (the case of Julliet Kairuki) Lakini dhana ya watu kulipwa bila kufanya kazi (wafanyakazi hewa) maana yake ni kuwa hakukuwa na kazi za kufanya ila maofisa wa serikali walikula njama ya kupanga malipo ya wafanyakazi wasiokuwepo/wasiohitajika (kazi isiyokuwepo) malipo husika wakawa wanajilipa wenyewe. Kwa hiyo hakuna albaki (si kazi wala pesa) katika dhana ya wafanyakzai hewa.
 
Sasa zoezi limefanikiwa ni wakati wa kuwaweka hadharani walokua wakila hizo fedha na pia kuyaweka hadharani majina hayo feki na mishahara yao.
Isije ikawa ni prop. Kama kawaida yetu
 
Jana rais kasema ni zaidi ya elf 10 ......tamisemi peke yake ni zaidi ya elf 8...
 
Back
Top Bottom