Wafanyabiashara wa sukari acheni unafiki

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,252
8,003
Tunakumbuka sana baada ya Rais Magufuli kupiga marufuku uingizwaji wa sukari kutoka nje mlikaa vikao na kujipongeza na kisha kumpongeza Mh Rais kufikia uamuzi huo!

Kinachoshangaza mlienda mbali zaidi mkakaa na bodi ya sukari nchini mkapanga na bei elekezi ya shilingi 1800@kilo, lakini kwa sasa mko kimya mnatufichia sukari hali iliyopelekea bei ya sasa kufikia Mara mbili ya bei elekezi ya awali.

Inawezekana kabisa mnafanya makusudi kuutega utawala wa serikali ya sasa kama ilivyokua kwa wafanyabiashara wa mafuta ya vyombo vya moto kwa serikali ya awamu ya nne.

BODI YA SUKARI NCHINI IVUNJWE, HAINA TIJA KWA TAIFA.

Hii bodi tangu hali ya upatikanaji sukari nchini kua mbaya iko kimya! Haioneshi msaada wowote kwa serikali kitu ambacho inatia shaka kwamba inashirikiana na Wafanyabiashara wa sukari kuhujumu uchumi wa nchi. Ni muda mwafaka kwa mamlaka husika kuimulika bodi hii haina tija yeyote.
 
Kwanza unahabari viwanda vimefungwa vipo kwenye ukarabati na ni utaratibu wa kila mwaka, alipipiga marufuku vibali alijipanga vipi?
 
Kwanza unahabari viwanda vimefungwa vipo kwenye ukarabati na ni utaratibu wa kila mwaka, alipipiga marufuku vibali alijipanga vipi?
Kama ndivyo ni kwanini bodi ya sukari haikumpa Mh Rais taarifa ili hatua zichukuliwe mapema? Bodi ya sukari nchini ni jipu lililovunda.
 
Bodi ya sukari wanakula mshahara wa bure kabisa.
Hakuna wanachofanya zaidi ya kutoa matamko baada ya matukio.
Hakuna uhaba wa sukari kwa sasa, wafanyabiashara wanatengeneza "scarcity" Ili wapige kwa kisingizio cha kwamba sukari haiingizwi kutoka nje.
 
Kwani lazima kunywa chai?waachieni wenye viwanda vya kutengeneza vinywaji n.k vinavyotumia sukari wanunue kwa hiyo bei yao
 
Nilichojifunza ni kwamba, kilimo cha sukari au uingizaji wa sukari nchini UNALIPA SANA, kama una mtaji.
 
Kama ndivyo ni kwanini bodi ya sukari haikumpa Mh Rais taarifa ili hatua zichukuliwe mapema? Bodi ya sukari nchini ni jipu lililovunda.

Tatizo maghu hajajua kuwa wasaidizi wake wengi wanataka ashindwe, isikilize kwa makini hotuba ya lissu, Kuna mambo maghu kwa kutokujua kwake anavunja sheria na huwenda serikali ikaja kushindwa kesi kwa kuwa hakufuata sheria
 
This is very dangerous!
 
Bodi ya sukari wanakula mshahara wa bure kabisa.
Hakuna wanachofanya zaidi ya kutoa matamko baada ya matukio.
Hakuna uhaba wa sukari kwa sasa, wafanyabiashara wanatengeneza "scarcity" Ili wapige kwa kisingizio cha kwamba sukari haiingizwi kutoka nje.
Sijui ni chombo cha nani hiki na ni kwa kazi gani!
 
Mbona mnafikiri upande mmoja?
Hivi magu aliwashauri kwanza au alitoa tamko?
Na kama alitoa unafikiri iyo bodi inauwezo wa kumkosoa?
Mi najua raisi anadhamira nzuri na nchi na bado ninaimani nae.
Akae vizuri na wachumi waliweke sawa ilo jambo
 
Back
Top Bottom