Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Shuguli kubwa za wakazi wa wilaya hiyo iliyoko pembezoni mwa barabara kuu ya Dar es Salaam –Mtwara ni biashara za aina mbalimbali, ambazo watu wanauza kutokana kwa wasafiri wa magari, nyakati zote, usiku na mchana.
Leo hii simulizi ya biashara hiyo imetoweka, hasa katika saa za jioni hadi usiku wote. Hiyo ni kutokana na agizo la serikali kupitia mamlaka za ulinzi, kutawaruhusu kufanya biashara usiku.
Kwa maana nyingine, wafanyabiashara hao hawako huru tena na ni hali inayosababisha wapoteze mapato yao ya kila siku. Kwa lugha, nyingine kiuchumi wameathirtika sana.
Hasara hiyo haishii hapo kwa wanaofanya biashara, pia hata kwenye vyanzo wanakochukua bidhaa hizo na o wamekosa soko. Ni hasara juu ya hasara.
Ni hatua ya kutetea usalama iliyochukuliwa baada ya matukio ya mauaji katika wilaya ya Kibiti na bado yana dalili za kuendelea kuwepo.
Ushuhuda kutoka Kibiti
Hivi karibuni nilibahatika kupita barabra ya Kilwa nikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Kibiti kikazi. Ilikuwa majira ya asubuhi na jionoi saa 12, nilirejea tena Dar e s Salaam kupitia nia hiyo hiyo.
Nilishuhudia namna vitongoji vilivyozoeleka kuona magari magari na abiria wake wakininua bidhaa mbalimbali, huku wachuuzi wakichangakka kukimbizana nayo, kufanikisha mauzo yao kwa, hali imebadilika sana.
Takriban vitongoji vyote vilikuwa kimya na hapakuwepo mtu hata mmoja anayeonekana hadharani.
Nilipjaribu kudadisi kuhusu ukimya ule, nilitaarifiwa na baadhi ya watu kwamba kila ifikapo saa 12 jioni huko Kibiti, watu wote hujifungia majumbani.
Wanasema kujifungia kwao ndani kunatokana na agizo la mamlak ya ua ulinzi za serikali, ikidai kuwatofanyika biashara kila ifikapo saa 12 jioni, hali
inayowafanya kila ifikapo saa 12 jioni, wanaingiza biashara zao ndani na wanye maduka nao wanafunga.
Kutoka Halmshauri Kibiti
Pia, wakazi wa Kibiti wanasema inapofika saa 12 jioni wasafiri wanaokwama, hulazimika kuomba hifadhi katika nyumba za wakazi jirani.
Ni hivi karibuni baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, walimuomba Mkurugenzi Mtendaji, Alvera Ndabagoya, awapatie vitambulisho vya kutumia, ili kuwahifadhi hadi siku inayofuata.
Madiwani hao walisemba mbali na kupatiwa vitambulisho, pia hata wakazi wa Wilaya hiyo nao wapatiwe vitambulisho, ambavyo vitawasaidia kuvionyesha pale wanapokutana na watu wa usalama kwa ajili ya kuwasaidia wasiwe wanasumbuliwa.
“Tunapokuwa na vitambulisho vinasaidia hata ukikutana na watu wa usalama unawaonyesha na wanakuachia, kuliko kutokuwa na kitambulisho. Hali hiyo inaweza kukusababishia unapokamatwa ukapata matatizo,” wanasema madiwani hao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, anasema gharama ya kutengeneza vitambulisho ni Sh. 14,000 kwa kila moja, ambayo bajeti ya Halmashauri haimudu.
Anasema uwezo wa Halmshauri ni kutengeneza kwa gharama ya Sh. 4,000 kwa kila moja na wameshampata mtengenezaji.
Mkurugenzi huyo aliwahakikishia madiwani kwamba vitatengenezwa, ndani ya kipindi kifupi wastani wa mwezi mmoja, ambavyo vitawarahisishia uhuru wao.
Mwenyekiti wa halmashauri, Khatibu Chaulembo, anawatahadharisha madiwani kutojadili suala hilo, na hadu sasa mwenye mamlaka pekee ya kulizungumzia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, amabaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa.
Pia anasema, kutokana na hali hiyo mbaya ya usalama, ukusanyaji mapato wilayani umeathirika kwa kiasi kikubwa.
Kilio cha wafanyabiashara
Baadhi ya wafanyabiashara ambao ni Mama Lishe na Baba Lishe, wanadai ufungaji wa biashara saa 12 jioni, umewaathiri kwa kiasi kikubwa.
Mwajuma Jumanne ni mmoja wao anayesema kabla ya matukio ya mauaji, hali ya kibiashara ilikuwa nzuri na anatoa mfani kwa siku waliuza hadi vyakula vilivyotumia mpaka kilo 10 za wali na kilo tano za unga wa sembe.
“Matukio ya mauaji yamechangia biashara kwenda vibaya. K siku tunapika kilo moja na nusu, hata hivyo kilo moja hiyo haiishi,” anasema.
Anaongeza kwamba kutokana na mabadiliko ya sasa, wameshuka hadi kutumia wastani wa kilo moja.
Mwajuma anaainisha kuwa soko kubwa la chakula huanza jioni, kuliko asubuhi na mchana.
Mwajuma anasema ‘kudoda’ kwa biashara kukwama na ameamua kuwaachisha kazi wafanyakazi wanne na kubaki na mmoja anayemudu kumlipa kila siku Sh. 3,000.
“Biashara ilipokuwa nzuri nilikuwa na wafanyakazi watano na kila mmoja alikuwa akipata kiasi cha shilingi 3.000 kwa siku. Lakini, baada ya kuona biashara haieleweki nimeona ni vyema kubaki na mtumishi mmoja ambaye nitaweza kumudu kumlipa,” anafafanua.
Wafanyabashara wa bodaboda, nao wanalalamika kupoteza soko kama ilivyo kwa wenzao Mama Lishe, ikizingatiwa kuwa biashara kubwa iko jioni.
Waliokuwa wakifanya biashara ya kuuza vinywaji baridi kama vile soda,juisi na vitafunwa nao wanatoa yao ya moyoni.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, wanalalamika kuharibika kwa biashara zao kutokana na zuio la safari na mzunguko ya kuanzia jioni.
Wanasema ni hali inayowatia uchungu, kwani wengi ni wadaiwa wa mikopo kutoka taasisi mbalimbali walizokopa na sasa wako katiika mtihani wa kushindwa kulipa.
Chanzo: Nipashe