Wafahamu Waadventista Wasabato

Ndio sabato yao inatakiwa kuwa Ijumaa sio Jumamosi
Vitu vingi wasabato wanaendana na waislamu kama kutokula nguruwe nk walitakiwa sabato yao wasali ijumaa kama waislamu wanaofanana nao wanavyosali
Hivyo vifungu kwenye picha umeenda kusoma? Maana hapo ndio pana hoja ya msingi.
 
Mwanzo 2:2-3
Sabato ilikuwepo tangu mwanzo ndugu yangu.
 
Kama msabato mstaafu, nikisema mstaafu namaanisha niliacha tu kwenda kanisani kwa sababu zangu binafsi wala si sababu za kikanisa, niseme tu kwa kifupi, hoja nyingi humu zinazopinga usabato hazina mashiko, katika watu wanaoyafahamu maandiko kinagaubaga namba moja ni wasabato. Kama unataka ufafanuzi wa kutosha tafuta msabato aliye iva kwenye maandiko peleka hoja zako, nakuhakikishia baada ya mazungumzo kuna asilimia 99 utakuwa msabato.
 
Mkuu naomba kuuliza je wasabato wa SDA huwa wanaadhinisha sikukuu ya Christmas
 

Wanayajua maandiko ila wamepotosha sana eneo la unabii hasa mamlaka ya papa wamechanganya uongo na ukweli ili kupoteza kondoo.

Pia dhana ya Yesu kuingia patakatifu pa patakatifu ni dhana ya uongo na si ukweli ilikuja baada ya hoja yao ya mwisho wa dunia mwaka 1844 kubuma.
 
Mkuu naomba kuuliza je wasabato wa SDA huwa wanaadhinisha sikukuu ya Christmas
Haipo popote hiyo.
Wewe fanya sherehe kila siku ama siku yoyote.
Kupotezeana muda tu huku mkiwapelekea fedha za kutosha siku hiyo eti mkidhani kuwa mnatoa shukurani,ni lini wao wamewaletea fedha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…