Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 2,365
- 8,631
Mwaka mmoja umepita tangu Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania, liomboleze kifo cha alieyekuwa Askofu Mkuu wa kwanza Tanzania (MWEUSI), MCH. YOHANA ZAKARIA LUSINGU...Mazishi yalifanyika nyumbani kwake, Suji, Same, Tanzania.
Injili ya Kisabato ilianza Tanzania mwaka 1903. Wamishenari wa kwanza kabisa kuleta injili ya Kisabato Tanganyika walikuwa; W. Ehlers na A. C. Enns ambao walitumwa na Union ya Ujerumani chini ya uongozi wa L. R. Conradi. Walifika Dar es Salaam December, 1903 wakaelekea moja kwa moja huko Upare kaskazini mwa Tanganyika (Tanzania).
WASABATO NI KINA NANI?
Nimeona vyema leo tuchambue kwa ndani juu ya watu wanaoitwa wasabato.
Wasabato ni watu ambao wanaheshimu na kuadhimisha siku ya sabato, jina lao linatokana na msisitizo wanaouweka kwenye kuiheshimu siku ya sabato. Pengine utauliza siku ya sabato ndo siku gani? Mbona katika lugha ya kishwahili hamna siku inaitwa sabato?
Neno sabato ni neno la Kiswahili lililotoolewa kutoka katika lugha ya kiebrania .
Katika lugha ya kiebrania neno hili linasomeka Shabbat lenye maana ya pumziko. Katika lugha ya kiebrania kuna siku inaitwa Shabbat, ambayo siku hiyo kwa Kiswahili inaitwa jumamosi. Angalia majina ya siku katika kiebrania na kiingereza,
English Name Hebrew "Name" Hebrew Meaning
kiingereza kiebraniia maana ya kiebrania
Sunday Yom Reeshone— First day
Monday Yom Shaynee —Second day
Tuesday Yom Shlee´shee— Third day
Wednesday Yom Revee´ee— Fourth day
Thursday Yom Khah´mee´shee— Fifth day
Friday Yom Ha´shee´shee —Sixth day
Saturday Shabbat— Rest
Kutoka kwenye neno Shabbat (sabato) , wote wanaoiheshimu na kuitunza siku ya sabato(jumamosi/Shabbat) wanaitwa wasabato.
Wasabato hawa wamegawanyika katika makundi tofauti kama ifuatavyo.
1. JUDAISM / WASABATO WA DINI YA KIYAHUDI
Hawa ni wasabato ambao historia yao ni ya kale sana . wanapatikana sana katika nchi ya Israeli , dini yao chimbuko lake ni katika biblia hasa agano la kale, Pamoja kwamba wasabato hawa wanaiheshimu siku ya sabato, jambo linalowatofautisha na wasabato wengine, ni kule kuamini kwao kuwa Yesu siyo masihi.
Wasabato hawa wa dini hii ya kiyahudi hawaamini kuwa Yesu ndiye Kristo/Masihi. Wanakubali kuwa Yesu alikuwepo ila hawakubali kuwa Yesu ndiye masihi aliyetabiriwa kwenye biblia agano la kale. Wao bado wanangojea ujio wa masihi atakayezaliwa ambaye atazaliwa Israeli na kuliongoza taifa hilo kuwa taifa lenye kuheshimika dunia kote.
Wasabato hawa wa dini ya kiyahudi wanashikilia msimamo wa babu zao ambao ndio walikuwa wapinzani wakubwa wa Yesu. Unaposoma katika biblia agano jipya utakutana na watu wanaitwa waandishi, makuhani na mafarisayo ambao walikuwa wakimpinga sana Yesu.
Imani ya watu hawa haikupotea ila waliendelea na Imani hii na sehemu kubwa ya wanachi wa Israeli waliendelea kuwa waumini wa dini hii. Hata Muisraeli asiyekuwa na Imani yoyote ujikuta akijumishwa katika Imani hii. Taifa la Israeli linasisitiza sana uadhimishaji wa sabato, sheria za nchi zinazuia kufanya shughuli kazi siku ya sabato, na mwezi wa kwanza 2018 bunge la taifa hilo lilipitisha sheria ya kuzuia biashara siku ya sabato (jumamosi).
2.WAKRISTO WASABATO/ KANISA LA KRISTO LA AWALI
Kundi lingine la wasabato ni lile la wakristo wa awali, Kundi hili lilizaliwa kutoka katika dini ya kiebrania au dini ya kiyahudi, Mwanzilishi wa kundi hili ni Yesu. Wafuasi wa mwanzo kabisa walikuwa mwanzo waumini wa dini ya kiebrania (dini ya taifa la Israeli).
Walikuwa wakisali pamoja na judaism katika masinagogi na mahekalu siku ya sabato (jumamosi) luka 4:16, matendo 13:42-43. Kutokana na kuamini kuwa Yesu ndiye Masihi/Kristo, kundi hili liletengwa na masinagogi ya kiyahudi (yohana 16:2). Jamii kubwa ya waumini wa kundi hili mwanzoni walikuwa ni wayahudi baadae wakaongezeka na jamii ya mataifa mengine. Wasabato hawa waliendelea kuiheshimu na kuiadhimisha sabato ( matendo 16:13).
Utunzaji wa sabato katika kundi hili ulikuwa tofauti na kundi lile lililo mkataa Yesu; wakati kundi lile lilizuia kuponya siku ya sabato (marko 3:2), kundi hili la wasabato-wakristo liliruhusu kuponya siku ya sabato, Wakati kundi lile lilisisitiza utoaji wa kafara siku ya sabato , kundi la wakristo- wasabato lilipinga utoaji wa kafara. Wakati kundi lile lilisisitiza tohara kama sehemu ya wokovu , kundi hili lilisisitiza tohara ya rohoni na ile ya mwili haikuwa na sehemu katika wokovu.
Makundi haya mawili yote yaliiheshimu sabato (jumamosi) lakini yalitofautiana namna ya kuiheshimu. Kundi hili la wasabato wa kikristo liliendelea kuwepo kwa wingi hadi karne ya tatu( 300 AD), Ambapo katika kusanyiko la Laodikia (Council of Laodicea 363-364) ilipitishwa kwamba wakristo wasiendelee kupumzika siku ya sabato / jumamosi badala yake wapumzike jumapili.( waweza soma wikipedia na vyanzo vingene vya historia kuhusu council of laodicea na malengo yake makuu).
Baada ya maamuzi haya waumini wengi wa kundi hili walihama na kuamua kuwa wajumapili (wanaopumzika siku ya jumapili) , Kundi hili la wasabato wakristo lilififia kiasi cha kuelekea kupotea kabisa maana yeyote aliyetaka kuendelea kuwa msabato alikabiliwa na mkono wa dola (selikali), mateso na kuuawa, ndipo wengi walijificha mapangoni na kuabudu kwa siri, kuendesha ibada za siku ya sabato ilikuwa kinyume na matakwa ya serikali ya Rumi.
3. SEVENTHDAY BAPTISTIST,
Kundi hili la wasabato ni matokeo ya vuguvugu la matengenezo huko nchini Uingereza katika miaka ya 1650. Matokeo ya matengenezo yaliyoibuliwa na Martine Luther mwanzilishi wa lutheran church katika miaka ya 1500 yalileta uamsho mkubwa wa watu kutaka kurudi katika misingi ya Biblia.
Japo martine Luther mwenyewe hakupokea fundisho la ubatizo wa maji mengi, wanamatengenezo waliofuata walikuja na fundisho la ubatizo wa maji mengi, Fundisho hili lilipelekea kuzaliwa kwa dhehebu la "Baptist church" katika miaka ya 1520, Ndani ya hili dhehebu lilijitokeza kundi lingine ambalo liliamua kurudi kwenye sabato ya biblia ambalo ni SEVENTHDAY BAPTIST (SDB). Viongozi wake wa awali kina Mr Andreas Fischer na mke wake walihukumiwa kifo mwaka 1520 na baadaye kuuwa. Wafuasi wa kundi hili walikuwa tayari kufa kuliko kuiacha sabato.
Oswald Glait ni miongoni mwa wahubiri waloisambaza sabato maeneo ya ulaya, hata hivyo naye alikamatwa na kutupwa mtoni. Kundi hili la Seventhday Baptist Church lilitambulika kama dhehebu na kufanya mkutano wake wa kwanza huko Uingereza mwaka 1651.
Kundi hili la wasabato halikufanikiwa kukua sana, Kwa sasa lina waumini karibu 50, 000 wengi wa waumini hawa wapo maeneo ya India na Marekani. Kutoka katika kundi hili la wasabato kulikuwa na muumini, mama mmoja aliyeitwa Rechael Oaks ambaye aliileta sabato kwa kundi la Waadventista na kupelekea kuzaliwa kwa wasabato tunaowafahamu waitwao SDA, WASABATO unaowajua Sasa, wale wa Kwaya zenye nyimbo nzuriii, kama vile Kurasini S.D.A Choir, Nyegezi S.D.A choir, Mbiu S.D.A choir, Magomeni S.D.A. choir, Sauti ya Jangwani Choir, Arusha Central S.D.A choir, Njiro S. D. A choir, Pasiansi S. D. A. Choir, Ambassadors of Christ Choir ya Rwanda, Golden Gate S. D. A choir Uganda, nk yaani nyingi mno... Bila kusahau Vocapella, Sonda ya Dihlu, nk
Hebu tuwatazame Sasa WAADVENTISTA WASABATO (SDA) niliowataja hapo juu👆👆
👇👇👇👇
4.WAADVENTISTA WASABATO (sda)
Kundi hili ndilo limeifufua sabato kwa kiasi kikubwa tangu ilipofifia enzi za mfalme Constantine na kuitawanya sehemu kubwa ya dunia. Kundi hili lilizaliwa rasmi kama dhehebu la kikristo mwaka 1863 chini Marekani.
Waanzilishi wake karibu wote walikuwa ni Wajumapili toka madhehebu tofauti kama Babtist church, methodist church kutokana na misukosuko waliyopitia. Baadhi yao ni kina Joseph Bates, James White, Ellen White na J. N Andrews. Hawa wote walipokea fundisho la utunzaji wa sabato kutoka kwa mama mmoja iliyekuwa msabato aitwaye Rechael Oaks aliyekuwa muumini wa dhehebu la SEVENTHDAY BAPTIST .
Waadiventista walilipokea fundisho la sabato na baadaye fundisho kuhusu sabato lilithibitishwa na maono ya Ellen G. White , binti ambaye kipindi hiki alikuwa akipokea maono. Binti huyu alipewa maono na kuoneshwa amri za Mungu kumi.
Na amri ya sabato ilionekana iking'aa sana. Kabla ya maono haya baadhi ya waadiventista walikuwa wameisha pokea fundisho la sabato na kulikubali na walikuwa tayari wameanza kupumzika na kufanya ibada siku ya sabato badala ya jumapili, E.G. White mwinyewe alikuwa amelipokea fundisho hili tayari.
Utunzaji wa sabato katika kundi hili unafanana kwa karibu sana na namna ulivyofanyika katika kanisa la Kristo la awali. Kundi hili hufanya oponyaji siku ya sabato, pia kutembelea wagonjwa na waitaji siku ya sabato ni jambo linaloruhusiwa. Kundi hili linaitunza sabato katika kumtazama Yesu na wanafunzi wake walichokifanya siku ya sabato.
Kama kuna shughuli yoyote ambayo Yesu aliifanya siku ya sabato basi shughuli hiyo ni halali kufanyika siku ya sabato katika kundi hili. Kundi hili la wasabato ndo kundi pekee miongoni mwa makundi ya wasabato ambalo limefanikiwa kukua na kusambaa duniani karibu kila nchi japo zipo nchi ambazo halijawa na uongazi lakini waumini wapo.
Kundi hili lina waumini zaidi ya milioni 20 duniani. Waadventista Wasabato (SDA) wana hospitali kubwa 198 duniani, vyuo vikuu zaidi ya 115 duniani na vituo vingi vya afya duniani, Wana shule za msingi na sekondari nyingi duniani.
Kwa ufupi nadhani umeelewa maana ya wasabato, na umefahamu makundi ya wasabato na tofauti zao. Somo hili liwasaidie wale wanaochanganya wasabato waliomkataa Yesu na wasabato wafuasi wa Yesu. Nikipata nafasi nitaleta historia inayopatikana.
(Marko 2: 27-28) Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia