Wafadhili Wapigeni Vita Viongozi wa CCM, Sio Wananchi
Kukata misaada kutoka nchi za magharibi (Marekani na Ulaya) hakuwadhurishi watawala lakini wanaodhurika ni wananchi. Watawala wanaendelea kupata mishahara yao minono, wanendelea kuiba na kunyang’anya na wanapokea chaochao yao kama dasturi. Anaekula hasara ni Mtanzania masikini atakaekosa kupatiwa maji na umeme, atakosa barabara mpya, watoto wake hawatopata shule mpya wala matibabu na mengineo pia.
Madola ya Marekani na Ulaya wameamua kukata msaada yao wanayoipa Tanzania kwa sababu ya uovu uliofanywa na serikali ya CCM katika kuvuruga dimokrasia visiwani Zanzibar. Jukumu la uharibifu huu linabebwa kwanza na Rais Magufuli na anasaidiwa kubeba mzigo wa fujo hili na Rais Shein.
Kwahakika Rais Shein hana hasara yeyote ikikatwa misaada au isikatwe. Yeye tonge yake inaendelea vilevile. Pia Wazanzibari hawana hasara kwa kuzuiwa au kukatwa misaada hiyo, kwani siku zote misaada hiyo haifiki Zanzibar na ilikua ikimezwa yote Tanzania bara. Watakao kosa misaada ya nchi za nje ni Watanzania bara. Hao ndio watakosa kila kitu.
Sasa ninapenda kuwaomba wafadhili wa Marekani na wa Ulaya wawonee huruma wananchi wa Tatanzania. Wasiwape shida wananchi kwa makosa ya viongozi wasiofikiria watu wao. Wakutiwa adabu ni viongozi sio wananchi.
Nini zifanye nchi za Wafadhili?
· Nchi za nje inatakikana wawazuie viongozi wa juu wa CCM kuingia nchi za Marekani na Ulaya.
· Pesa za viongozi wa CCM zilioko kwenye mabenki ya nje zizuiwe na zikamatwe.
· Zitolewe amri za kuwakamata na kuwahukumu wakipatikana.