Waeleweni wake zenu

Waeleweni wake zenu

happiness win

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
2,461
Reaction score
1,394
Jamani wanaume jitahidini sana tena kwa bidii kuelewa wake zenu wanataka nini kwenye ndoa. Kuna wanawake wanaoolewa wakitaka mapenzi tu, kuna wanaotaka pesa na mapenzi, kuna wanaotaka kutoa mikosi kwa kuolewa, kuna wanaotaka watoto tu, kuna wanaotalii kwenye ndoa, kuna wanaotaka ndoa kikweli kweli, kuna wanaotaka hifadhi tu, kuna wanaoolewa kwa sababu wamekuta utamaduni huo na mambo mengi ambayo utayajua ukiwa makini kujua mkeo anataka nini.

Hivi umeshawahi kufikiria mkeo anataka nini?

Na wewe mwanamke ushawahi kufikiria kwa nini umeolewa au utaolewa na unataka nini kwenye ndoa?

Fungukeni wandugu.
 
Tujuze kwanza we umeolewa au bado ili tuje na majibu.
 
hii inaweza kuwa na ukweli lakini jinsi ganiutajua sababu ya mwenza kutaka kuingia kunako ndoa? manake nahisi ni muhimu kujua sababu kabla hujaingia ndoani.
 
happiness win
Kuna wanaotaka kuwa na maisha yao binafsi yenye heshima na maamuzi, anaamini akiolewa anaenda kuwa na mamlaka katika mji wake anaokwenda kuuanzisha na kuiongoza vyema familia yake!!
 
Last edited by a moderator:
LET ME PUT YOU ON THE GAME CUTE BOY! How does it feel to be on the MENU? Jiwe limerushwa gizani! USITHUBUTU KUPITWA NA BWANA PEPSI HUYU! Hahahaaaaaa!
 
Sisi tulioana kwa sababu tulipendana na hatukutaka kuchezeana wala kuumizana na kuachana,tulihitaj kujitegemea na kujenga familia yetu
 
Natoa mchango wangu sasa! Sio uwongo uyasemayo! Ila mimi i believe peoples interest change over time! Huenda ni kweli alipoingia ndoani alikuwa anataka hivo, lakini with age,life experiences, na exposure tunavovitaka vinabdilikaaaa!

Kama mimi what i wanted when i was 21 ni tofauti kabisaaaa na what i want now! Na kuna ragiki yangu ali devorce 24 saivi yuko na mwanaume mwingine anakubali divorsing the first guy was a mistake and unreasonable! Same person but more matured ideology!

The thing is kujaribu. Kwenda pamoja intrest zikiwa zinabadilika!
 
Kuna wanaotaka kuwa na maisha yao binafsi yenye heshima na maamuzi, anaamini akiolewa anaenda kuwa na mamlaka katika mji wake anaokwenda kuuanzisha na kuiongoza vyema familia yake!!

Sawa kabisa. Sasa mtu kama huyo atakapofika kwenye ndoa na kukuta heshima aliyoitarajia haipo, mamlaka hana inakuwa balaa. Ila akivikuta ndoa inakuwa mwake mwake!
 
lara 1

Nime-fall in love kwenye comments zako! Umenena vema.
 
Last edited by a moderator:
Hapo chacha ujue jinsi ya kuwatimizia. Dudu mara tatu kwa siku hapo hapo ukafanye kazi upate pesa za kutosheleza mahitaji yake, umuwezeshe utalii ndani ya ndoa, yaani...... utakufa siku si zako
eeee kufa tena .....??? kwaheri
 
Jamani wanaume jitahidini sana tena kwa bidii kuelewa wake zenu wanataka nini kwenye ndoa. Kuna wanawake wanaoolewa wakitaka mapenzi tu, kuna wanaotaka pesa na mapenzi, kuna wanaotaka kutoa mikosi kwa kuolewa, kuna wanaotaka watoto tu, kuna wanaotalii kwenye ndoa, kuna wanaotaka ndoa kikweli kweli, kuna wanaotaka hifadhi tu, kuna wanaoolewa kwa sababu wamekuta utamaduni huo na mambo mengi ambayo utayajua ukiwa makini kujua mkeo anataka nini.

Hivi umeshawahi kufikiria mkeo anataka nini?

Na wewe mwanamke ushawahi kufikiria kwa nini umeolewa au utaolewa na unataka nini kwenye ndoa?

Fungukeni wandugu.

mwanaume ataachana na wazazi wake ataambatana na mkewe, nae mwanamke ataachana wazazi wake ataamba na mumewe, nao watakuwa si wawili tena bali watakuwa mwili mmoja.

Huu ndo msingi wa ndoa kwetu sisi wakristo. Hayo yote uliyotaja ni ya shetani ndo maana yanavuruga ndoa nyingi.
 
wa siku hizi wanaolewa ili kuondoa mikosi. akishaiondoa na watu wakaacha kumsema anaanzisha varangati na kuvunja ndoa.
 
Back
Top Bottom