Wadau msaada wenu tafadhali, I have a hard times

nina nchi sita

JF-Expert Member
May 23, 2016
269
141
Naitwa ngosha(jina la utani) naishi songwe (mkoa mpya)

Nilipo fikia umri wa barehe nilianza kugundua vitu flani .kwamba mbona wenzangu wanapata madem kiurahisi lakini kwangu inaniwia vigumu sana kuwapata viumbe hawa. Najiamini sana kuwaeleza hisia zangu lakini naambulia patupu. au kwa sababu natoka familia ya kimaskini..?. Lakini hapana mbona vijana wenzangu wanapendana bila kujali hali zao?

Nikafikia umri wa miaka 20 nikiwa cjawahi Ku sex. Hapo nikagundua jambo flani. Mtaani watu walikuwa wakiniita fid q(enzi hizo fid q alikuwa na sura mbaya sana) mala nikaanza kuitwa mjukuu wa mizengo pinda.afu kuna dem mmoja alikuwa anaitwa pendo watu walikuwa wanadai hajawahi kukataa wanaume ni ww tu na kujieleza kwako. Mda huo nilikuwa cjatongoza mda mrefu kutokana majibu ya kukatisha tamaa niliyo kuwa nikipewa. nikajisemea ngoja nijaribu kwa pendo. Baada kujieleza tu kuwa nampenda, pendo alinipa jibu lililo nifungua akili. Maneno aliyo nijibu hayajanitoka kichwani hadi Leo

Alisema "ntakupeleka wapi wewe na sura lako bovu ka fenesi na pesa huna

Nikiwa nyumbani nikajitathimini nikiwa mbele ya kioo huku majina yangu ya utani nilopewa mtaani yakijurudia.nikajua hakuna haja ya kubishana na ukweli nilioambiwa na pendo. Coz ni kweli tupu.

Hapo nikaacha kabisa kufuatilia habari za wanawake. Kwa kuwa elim yangu ni std7 ikabidi nikomae tu na kazi ili walau niwe na pesa inipe ka uhb. Pia nikawa najitahidi kuwa msafi mda mwingi ili walau nione kama ntawavutia viumbe hawa

Nilifaulu kiasi flani. Nikawa nang'oa baadhi maduu. Nikawa nikiwapata nafanya kadri niwezavyo ili ujuzi wangu wa kitandani uwavutie hawa watu. Nilianza kutembelea blogs na website mbalimbali ili kujifunza namna ya kumpagawisha mwanamke kitandani. Kwa asilimia flani nilifaulu katika hilo.

Moyoni Nikamshukuru pendo kwa kunifanya nijitambue.

Tatizo likawa kwamba cjawahi kuwaamini wanawake hata cku moja. Kwani niliamini hawakunipenda Mimi bali elf5 tano na ten ten nilizo kuwa nikiwapa

Bado nilikuwa na mtihani mkubwa saana wa kujijenga kimaisha

Nilikuwa nafanya kazi katika kiwanda kidogo kilichokuwa kikizalisha Keki.

Hapo kuna dada mmoja alikuwa anaitwa trace.alikuwa mzuri mno. Mwepe. Umbo no nane macho makubwa ya mviringo. Kwa kifupi alikuwa ni mrembo mnoo. Akikuwa anasoma yupo 4m 4 wakati huo.baba yake ni MTU maarufu na mwenye pesa kibao. yaani kwa kifupi kwao dhiki wanaiskia maredion

Kila asubuhi ilikuwa n zam yangu kukaa katika kibanda cha mauzo ya Keki, na kila asubuhi ilikuwa lazima trace aje kununua keki kwa ajili ya chai ckujua kwa mini alikuja yeye mwenyewe kwani nyumbani kwao wafanyakazi kibao.

Japo mwanzo nilikuwa nikimuogopa, nikaja kugundua kuwa trace ni msicha mmoja simple saana. Hivyo nikazoeana nae saana mpaka. Washkaji zangu wakampa jina la Mrs fid q

Ilikuwa jioni ya ijumaa siku hiyo mshikaji wangu akaniomba nimshikie zam yake coz alikuwa ana promise na dem wake koo nikabaki ofisini.

Mida flani hivi ya jioni nje ya ofisi yetu, gar aina ya Noah ikapaki kisha trace akashuka kwenye gari akiwa na mshikaji flani hivi shombe shombe. Haikuwa na haja ya kujiuliza. walikuwa ni wapenzi. Trace alikuwa ameshika zile pombe zinazokuwa 6 in1. Wakaongea maneno kadhaa kama wanaaga kisha wakapigana makiss then jamaa akaingia kwenye gari huku trace akimsisitiza asichelewe.

nilijijua tu kuwa siwezi kummliki trace lakini jinamizi la wivu lilinitesa saana. nilitamani ningekuwa na pesa au HB kama jamaa ili na mm nipate hata chance ya kumkiss trace. Ia nikajiona naota ndoto mchana

Trace akaja mpaka ofisini Petu. Akaomba siti nikampa.akakaa huku akinitania akiniambia Leo anataka kukupiga msasa mpka uitwe mtanashati

Mda ulisonga na shombe shombe hakurudi trace akawa anapiga mala nyingi saana kumuuliza jamaa kulikoni mbona anamuweka saana mwishowe simu ikazimwa. Trace akaaza kuzigonga zile six pac mpaka akalewa.

Mda wa kufunga ulipofika nikamwambia trace, nataka kufunga, koo asepe. Cha ajabu akanambia kwao ameaga anaenda mbali, pia hawezi kurudi akiwa amlewa. Nikamshauri akalale kwenye nyumba za wageni. akanambia hana pesa coz pesa zote shombeshombe kasepa nazo.

Duh nikijicheki cna mpungu zaidi ya mpunga wa ofisi. Kwa kuwa nilikuwa namuamini nikasema basi ntakuazima.

Akanambia wee vipi kwani kwako hupokei wageni.

Duh nikapigwa na butwaa trace ni mwanafunzi, mtoto wa kishua, afu kalewa, ghetto kwangu Mali ya thamani kuliko zote godoro la 6/4 limelazwa chini, na visefuria vichache vya kupikia yaaaani duh full msala

*******************"********
*******************

Trace mpaka naingia nae ghetto six PAC imebaki na 1pac. huku nimeuviringisha mkono wake mabegani kwangu. Nikambwaga kwenye kigodoro changu. Ile anajiweka sawa nikashangaa anapiga kwi kwi Mara huwaaaaaaaaaaa akarudisha chenji. Ghetto zima hovyo nakajiambia huu msala sasa. Afu ile kipombe pombe akanambia "fid pole mtu wangu" kisha akajibwaga kwenye kigodoro changu huku kisketi chake kikiacha mapaja yake mazuri yaonekana. Maskini trace kajitapikia mpaka kwenye sweta alilolovaa ikabidi nimvue ili asichafue godoro.

Nikamlaza vzr then nikamfunika, kisha nikafanya usafi mdogo mle ndani. Moyoni nikaazimia kutofanya chochote kwa trace bila ridhaa yake na hata ikiwa ni ridhaa yake nisingeweza coz pombe ndio ingekuwa imeamua na si yeye.

Pia nikawaza trace kwa uzuri wake amgeumia saana endapo kesho yake akiwa mzima angegundua amesex na mm. Basi nikajisogeza nikalala na kujifunika shuka.

Usiku nikiwa nimelala nikashangaa najihisi kama nimelala kwenye dimbwi la maji. kuvuta harufu nikagundua n mkojo. Maskini trace alikuwa amekojoa mkojo mwingi hatare. Yaaani ikabidi nijilaze miguuni tena bila shuka manake lilikuwa limelowana.

Usingizi ulikuwa wa mang'amung'm cku hiyo kufikia saa 10 alfajiri usingizi ukawa umekata kabisa. Bas nikaamka nikaanza kufanya usafi magheto trace akiwa amelala nikafua mpaka mashuka hali ya ghetto ikawa safi likabaki godoro tu.

Kufikia saa 12:00 nikwa nimeshaa andaa maziwa fresh na chapti zikawa tayari ikabidi sasa nimuamshee trace. Cha ajab baaada ya kumuamsha akaniomba nimuandalie maji ya kuoga. Ckuwa na hiyana nikafanya kama alivo taka. Baaada ya kuoga kwenye mabafu yetu haya ya uswahilini, akanywa chai, kisha akaniomba nguo avae coz zake chafu. Nikampa jinzi na t shart akavaaa kisha nikamwambia nataka niwahi kazini. Akadaii yeye ataondoka mchana ivo nimuachie ufunguo na kufuri atafunga. Nikafanya kama alivotaka nikawahi zangu kazini

Mpaka Leo cjuagi kwa nini nilijiamini kiasi hiki kwa huyu mwanafunzi mtoto wa kishua.

*************************

Basi cku ile nakumbuka ufunguo nililetewa na mfanya kazi wa akina trace ila tangu hapo mpaka trace anaenda arusha kwa masomo ya advance ckuwahi kumtia machoni teeeena. Mpaka anaaaanza chuo mwaka wa kwanza na wa pili

Sasa nikaachana kazi ya Keki nikaenda zangu dar kusaka maisha. Nikawa nafanya kazi ya kuziba pancha pale mbagara mbagara rangi tatu.

Ki ukweli kutokana na ugumu maisha ilikuwa vigumu sana kumpata msichana aliekubari kujenga malengo na Mimi na hili sura langu ka fenesi. Roho iliniuma saana nilipokuwa nawaona wenzangu na wapenzi wao. Nilijiuliza Mimi binadam wa aina gani, pesa sina, sura mbovu, elim std7, ntafanyaje na maisha haya ya hivi upweke daily.

Siku moja nikiwa nafungua tairi ya gari ili niizibe pancha. Nikaskia sautiii ya like ikiita pindaaaaaaa. Nilijiuliza pinda mimi ama uku DSM kuna RAIA mwingine kapewa jina kama langu. kugeuka huvi ckuamini macho alikuwa ni trace!!!

Trace alinikimbilia nilipo na bila kujari uchafu wangu akanirukia na kunikumbatia kwa nguvu. Nikabaki nimeduwaaaa cjui nifanyaje. Raia full kutukodolea mimacho. Trace hakujari hilo. Trace alipo niachia ile kumuangalia usoni, heeeeee!!!!!! mchozi unamtoka nikatamani kumfuta, mikono michafu, nikabaki namuangalia nisijue cha kufanya. trace hakuongea mengi aliniomba no ya simu nikampa akaondoka huku akiahidi kunitafuta.

Kwa takribani miaka mi4 abayo cjaonana na trace, trace amekuwa mrembo mla dufu. Nikatamani awe mpenzi wañgu lkn nikajiambia mi sio tyep yake

Ni jmos nipo kazini ila sio kikazi nilijitahidi kuvunja kabati kadri ya uwezo wangu. Nilikuwa namsubiri trace kama tulivyo ahidiana kwenye cm. Trace alifika na bajaji nilipomuona akishuka nikamfuata nimpe mkono wa l salam lkn trace alinihug den akanikiss shavuni. Jamani acheni trace alinifanya nijihisi kidume kwa

Trace alinizungusha maeneo kibao dsm ambayo nilikuwa siyajui. mda wote tukiwa matembezi trace hakuogopa MTU yeyote alionyesha mapenzi yake hadhalani bila kujari aliniñikiss, alinihug, alinishika mkono.

Mda mwingine nilijikuta namkumbatia trace huku machozi yakinitoka ckuamini trace na urembo wake amenipenda mimi mtoto wa kimaskini

*****************************

Tulifika nyumbani kwa akina trace baada ya yeye Ku hitim masomo yake ya chuo ili anitambulushe kwa wazazi wake nilikuwa na woga sana. Maskini asiye na elim kama mm ntaongea nini mbele ya kibosile. Lakini cha ajabu mzee pamoja na mkewe walinipokea kwa shangwe sana tofauti na nilivo dhania. Hakika nilijiona mwenye bahati

Kesho yake Trace akaniletea zawadi kwenye box kufungua nikakutana na zile nguo nilizo muazima kipindi kileeee alipo lala ghetto tulifurahi saaaaaana. Jioni mida ya saa mbili hivi Nika msindikiza kwao

Baaada ya kumsindikiza Wakati narudi njiani nikiwa napita pembeni ya Barbara kulikuwa na gari imepaki mala mlango wa ile gari ukafunguliwa wakatoka wababe watatu wakanikwida na kuniiingiza ndani. Ya gari. Wakanipa chai kisawia kisha wakapiga simu nikaskia wakisema "tunaye hapa ashawiva kisaiwia" kisha wakanipa ile simu nikaskia Sauti upande wa pili ikisema. Chaguo ni lako uendeleee kuishi au ufe kwaa sababu ya kumga'ang'ania trace" simu ikakatwa. Sikuwa na haja ya kujiuliza sauti ile ilikuwa ya baba ake Trace. Baada ya kuongea na n cm wale jamaa wakanitoa nje ya gari wakasepa

*****************************

Sasa hivi in cku ya NNE tangu tukio la kipigo linipate na sijaenda hosptl namshukuru mungu naendelea vzr

Nilimdanganya kuwa nilipigwa na vibaka. Nikagoma kàbisa kwenda hsptl kwa madai kuwa tutaaaanza proces nyingi police station na akanielewa

Kwa kweli sasa hivi nayaona kabisa mapenzi ya trace. Akili yangu inagoma kabisa kumwacha trace coz czanini kama ntampata mwingune kama yey

Najiona nipo tayari kufa sio nimkose

Nipo njia panda wadau cjui cha kufanya msaaada wa kimawazo Tafadhali
 
1. Kichwa cha habari tu kinachosha
Achana na "Englishes " andika tu kiswahili mkuu.
2. Mpangilio wa masimulizi yako mbovu na unachosha akili (kwa walio timamu). Ndo maana wachache sana wanaweza kusoma mpaka mwisho.
NB. Memkwa wanapokea watu wazima kwa ajili ya kujifunza mwandiko (sina nia ya kudhalilisha mtu, ni ushauri tu)
 
1. Kichwa cha habari tu kinachosha
Achana na "Englishes " andika tu kiswahili mkuu.
2. Mpangilio wa masimulizi yako mbovu na unachosha akili (kwa walio timamu). Ndo maana wachache sana wanaweza kusoma mpaka mwisho.
NB. Memkwa wanapokea watu wazima kwa ajili ya kujifunza mwandiko (sina nia ya kudhalilisha mtu, ni ushauri tu)
Ntaufanyia kazi mkuu subir nipone
 
1. Kichwa cha habari tu kinachosha
Achana na "Englishes " andika tu kiswahili mkuu.
2. Mpangilio wa masimulizi yako mbovu na unachosha akili (kwa walio timamu). Ndo maana wachache sana wanaweza kusoma mpaka mwisho.
NB. Memkwa wanapokea watu wazima kwa ajili ya kujifunza mwandiko (sina nia ya kudhalilisha mtu, ni ushauri tu)
Umelazimishwa kusoma hapa unaweza kausha tu ukapita kimy kuliko kutoa ushaur wako uchwara wenye kebeh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom