Wadada Ndivyo Sivyo

Anapenda watu wenye shida.. ili awaendeshe vile anavyotaka yeye..
 
Sitaki kuamini. Yaani mwanamke kwenye raha ndio hamtaki mwanaume.

Ni katika dunia hii tuliyonayo ama nyingine.

Lazima kuna kitu nyuma ya pazia
Amini na inawezekana kabisa.

Mimi nilikuwa na mpenzi wangu, nilikutana nae akiwa na kazi nzuri hivyo sikuwahi kupata shida nikiwa nae, alinipa kila kitu, ni mwanaume ambaye siwezi kumsahau katika maisha yangu.

ghafla ile kazi ikaisha, ikawa kila kitu nafanya mimi, majukumu yote ya familia, nilizidisha kumpenda zaidi ya mwanzo, tena sana kilichotokea ndugu yake akawa anasema nilimpendea pesa tu hivyo lazima nitamuacha, sikufanya hivyo nilijitahidi hata nikipata pesa nampa zote yeye ndio aamue cha kufanya.

Baadae akapata kazi nzuri zaidi ya ile ya kwanza na akaniambia sasa mama huu ndio wakati wako utasahau shida zote.

Huwezi kuamini hapo ndio nilimuacha. Sio kwamba sikumpenda ila nilichogundua ndugu yake hakunipenda kabisa tangu mwanzo. Pia alidhani nimempendea pesa. Sasa niliamua kumuacha akiwa ana pesa zaidi ya mwanzo
 
Nna wasiwas huyo mwanaume alianza kubadilika demu akaona isiwe shida akasepa
 
Sababu hasa ya kumuacha? kwani unaishi na ndugu yake au na yeye?
 
Unaamini kweli ulikua unampenda wakati unamuacha?

Unaamini kuwa ulimuacha kwa sababu ndugu yake hakukupenda?

Endelea kujidanganya lakini tafadhali usitudanganye.
 
Umeongea ukweli mtupu, shida ipo kwa mwanaume
 
kwahiyo wewe unaishi na mume kwa kupendwa na ndugu zake? hata wewe hukua muaminifu unalazimisha kupendwa na asiyekuoa
 
Unaamini kweli ulikua unampenda wakati unamuacha?

Unaamini kuwa ulimuacha kwa sababu ndugu yake hakukupenda?

Endelea kujidanganya lakini tafadhali usitudanganye.
hata mimi sijaelewa kwahyo mke wangu aniache kisa kaka yangu hampendi dah anataka ampende ili amfanyeje
 
Kumdefine mwanamke ni ngumu sana kwa sabab definition yao haisomeki kwa lugha yoyote na kila taifa wanalia na kuwadefine hawa viumbe
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…