Acheni kulaumu wanawake, niwewe mwenyewe mwanaume katika kuchagua kwako, na unaona toka mwanzo anakupiga mizinga, unamzoesha tu.
Mambo ya hela yakienda kombo ndio unaanza lalamika na kuona hilo kwa macho mawili.
Sijui hao wanawake wako wapi wa kupiga mizinga mara zote.
Anzisheni kampeni ya tokomeza mizinga labda wenye tabia hiyo, wataona aibu.
Pia tatizo la kutokubaliana mapema mkiwa mnaanza mapenzi, lazima mjadili hayo yote ikiwemo suala la hela.
Daah! jamani hii ni hatari yaani usimzoee mdada kidogo tu hata hujamtongoza kashaanza kukupiga mzinga mara ninunulie simu, hela saloon, mara weekend twende wapi! mara mama anaumwa naomba uniongezee hela ya dawa.
Kina dada hali yenyewe si mnaiona jamani?
Mbona mnataka tuwe wezi bila kutaka?
Tena kama ndo sikupendi utajuta
Afu kuna mtu humu mda si mrefu najiandaa kumwomba laki 6 nina shida nayo najua umesoma ujumbe huu jiandae .thanx in advance