uwe hodari
JF-Expert Member
- Dec 16, 2022
- 4,041
- 8,633
Ukristo duniani kote unaendeshwa kwa upendo,amani na kuvumiliana
Ila wachungaji wa makanisa binafsi wanafanya mambo yaliyovuka kiwango cha ibada na kuonekana zaidi kama wanafanya vituko
Naamini wachungaji wengi walikuwa na lengo la kumtumikia na Kutangaza injili ya krstu walipoanza malengo yao ila kwa namna moja ama nyingine wengi wamepotoka njiani na kuanza kufanya ujinga na vituko kanisani
Nilimsikia dada mmoja anajiita mchungaji anahubiri yeye ni mchungaji akiwa kanisani tu ila akiwa chumbani anayaachia yote km mwanamke
Nikijisikia vibaya kwa kweli kuhusu ile clip kwasababu kwa mazingira pale walionekana wapo kwenye Ibada
Ingelikuwa wapo kwenye semina ya ndoa angeyazungumza hayo wala isingekuwa ajabu kwasababu angekuwa anakutana na watu wanaojiandaa kuingia kwenye ndoa
Imagine umejiandaa jumapili kwenda kwenye ibada unakutana na dada mmoja mpuuzi km huyu anahubiri sex kwenye saa za Ibada takatifu
Niliona yupo comfortable kabisa kwasababu ule umma wa waumini wake waliokuwa wanamsikiliza hawakuonesha reaction ya kutokupenda maongezi yake yasio maana
Niliona Pia clip nyingine mchungaji anawalisha matango waumini wako eti
"mwaka 2024 utakuwa mwaka wa mafanikio kwasababu unagawanyika kwa mbili"
Ni mchungaji fulani alikula suti yupi calm kabisa anaropoka haya
Sasa nukajiuliza ni wapi Biblia Takatifu imenukuu miaka ya neema kuwa ni ile inayogawanyika kwa mbili?
Ni bora hata angekusia kuhusu mstari ya Biblia Takatifu kuhusu miaka Saba ya neema na Miaka saba ya njaa ( kuwa maisha yamegawanyika ktk vipindi viwili kwenye kila jambo)
Lkn yeye aliishia kusema tu mwaka 2024 utakuwa mwaka wa mafanikio kwa kuwa unagawanyika kwa mbili
Bahati mbaya mpiga picha hakuonyesha waumini wake nione muitikio wa ile kauli
Kiufupi huyu mchungaji aliokota maneno ya mtaani tu kuhusu assumption zake
Haya makanisa binafsi mengi yanaenda ili mradi hakuna litrujia
Mchungaji anaanza kuongea saa nne asubuhi hadi saa tisa alasiri? Inahuruma nini zaidi ya kusababisha watu waanze kusinzia kanisani? Na maana ya ibada kutopotea?
Kila kitu kina utaratibu wake tengenezeeni mpangilio wa ibada mnaboa kwa kweli
Wengi wa wahanga wa hizi ibada ni wanawake wanaondoka na watoto nyumbani asubuhi kurudi nyumbani usiku
Wakristo wengi hawajui km kuomba na kujiombea binafs kuna nguvu sana kuliko kwenda kupokea mafundisho ya sio na kichwa wala miguu kwa wachungaji watafuta riziki
Kwanza mwanamke unakuwaje mchungaji?