Kweli hata mimi huwa inanikera sana. Hiyo ya kukaukiwa pointi huwa wanaificha kwa kurudia mara nyingi "Bwana asifiwe!" mkijibu "Ameni" wanajifanya sauti ndogo wanarudia tena na tena mpaka tunachoka.
Wakati mwingine utasikia mwambie mwenzako "uko nyumbani mwa bwana" siku moja nikamgeukia kumwambia mwenzangu kumbe alikuwa ameuchapa usingizi ikawa kama nimemsitua akaruka nusu aanguke.
Wajaribu kuwa na mahubiri mafupi wakati mwingine wanayarefusha bila sababbu kwa kurudia rudia vitu walivyokwisha kuvisema. Asante. "Bwana Mungu asifiwe sana!"
Hilo la sadaka ndio balaa. Utaambiwa shukurani ya siku ya bwana, uwakili na jengo, sadaka ya misioni, mkutano mkuu, safari ya kwaya kuu, ununuzi wa sare za kwaya ya vijana inayokwenda kurekodi albam, maji kwa ajili ya safari ya kwaya, ugeni wa kutoka dayosisi, ujenzi wa ngazi za ofisi ya mchungaji, fungu la kumi, shukurani ya pekee, shukurani ya matukio, sadaka ya meza ya bwana, sadaka ya faraja nk nk ili mradi ni mizunguko mingi ya kwenda mbele kutoa sadaka kuna siku teulikwenda mizunguko mitano. Jamaa yangu mmoja alikuwa mjanja akachenji 1000 kuwa 200 ili aweze kukamilisha mizunguko kwani ukiuchuna kwenye kiti bila kwenda unajisikia aibu na wakati huo huo watumishi wanakuona. Hii ndio imesababisha siku za jumapili watu wanapokwenda kwenye ibada kuanza kuhangaika na kuchenji hela njiani hadi wengine kuchelewa ibada. Sasa kama mko watatu au watano katika familia inabidi mtafute chenji za kutosha kulingana na mizunguko. Bora sadaka ingekuwa moja tu mtu ukatoa buku na kuishia. Hii ipo sana kkktmi naabudu huko! huwa sigeuki maana haina mwongozo wowote kwenye bible. wanatuzingua kwa mengi hawa jamaa. Mara utakuta ibada moja sadaka awamu sita wameambiwa waumini ni viwanda vya kufua pesa!
uwekwe utaratibu please!
Hilo la sadaka ndio balaa. Utaambiwa shukurani ya siku ya bwana, uwakili na jengo, sadaka ya misioni, mkutano mkuu, safari ya kwaya kuu, ununuzi wa sare za kwaya ya vijana inayokwenda kurekodi albam, maji kwa ajili ya safari ya kwaya, ugeni wa kutoka dayosisi, ujenzi wa ngazi za ofisi ya mchungaji, fungu la kumi, shukurani ya pekee, shukurani ya matukio, sadaka ya meza ya bwana, sadaka ya faraja nk nk ili mradi ni mizunguko mingi ya kwenda mbele kutoa sadaka kuna siku teulikwenda mizunguko mitano. Jamaa yangu mmoja alikuwa mjanja akachenji 1000 kuwa 200 ili aweze kukamilisha mizunguko kwani ukiuchuna kwenye kiti bila kwenda unajisikia aibu na wakati huo huo watumishi wanakuona. Hii ndio imesababisha siku za jumapili watu wanapokwenda kwenye ibada kuanza kuhangaika na kuchenji hela njiani hadi wengine kuchelewa ibada. Sasa kama mko watatu au watano katika familia inabidi mtafute chenji za kutosha kulingana na mizunguko. Bora sadaka ingekuwa moja tu mtu ukatoa buku na kuishia. Hii ipo sana kkkt
Wengine wanazidisha bwana. Mara mgeukie mwenzako mwambie "umekombolewa" kidogo tena "mwambie bwana anakupenda" mara "uko hemani mwa bwana" tena "shetani ameshindwa" ghafla "leo ndio siku yako bwana aliyokupangia" wakitoka hapo utasikia "shangilia na piga makofi kwa bwana" "vigelegele akina mama" ... Wakati mwingine mbwe mbwe nyingi kuliko mahubiri yenyewe. Unaweza kukuta mahubiri yenyewe ni ya dakika 15 atakwapeleka mpa masaa 2Punguza jazba uingiapo hemani mwa Bwana. Hizo ni tacts za kufundishia
Ameni!Hivi ulishawahi kulazimishwa kutoa sadaka!? hautaki usitoe pia acha kwenda kanisani. uone kama huduma zitasimama. sio kuja kulalama hapa jf