Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
RAIA watatu wa China, wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh milioni nne kila mmoja baada ya kukiri kukwepa kodi ya Sh 350,000 kwa kutumia mashine za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs).
Raia hao ni Liu Songyue, Liu Pengfey na Jiang Zedong ambao ni wamiliki wa Kampuni ya M/S Sen He CO Ltd , waliofikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jana. Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan alisema hawana kumbukumbu ya makosa ya awali kwa washitakiwa.
Alisema kwamba sheria ya kodi, inaruhusu washitakiwa wenye makosa kama hayo, kulipa faini, kifungo au vyote kwa pamoja. Alisema kutokana na washitakiwa kukiri makosa yao, watatakiwa kulipa faini ya Sh milioni nne kila mmoja au jela miezi sita.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa washitakiwa, Nahimia Mkoko, aliiomba Mahakama iwape washitakiwa hao, adhabu ya kulipa faini kwa kuwa serikali ipo zaidi kukusanya mapato. Alidai washitakiwa wakilipa faini, mapato wataendelea na shughuli zao na kwamba wataendelea kulipa kodi vizuri kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Awali, akisoma mashitaka hayo, Wakili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Marcel Busegano alidai kuwa washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka ya kutoa taarifa za uongo kwa Kamishna. Busegano alidai washitakiwa walitenda kosa hilo kati ya Machi 12, mwaka huu, maeneo ya Tabata Shule wilayani Ilala katika Kampuni ya M/S Sen He CO.
Ltd chumba namba 11,12 na 13. Alidai kuwa washitakiwa walitoa risiti ya mauzo kwa mteja, Mwise Wambura ya Sh 200,000 kutoka kwenye mashine ya EFDs inayomilikiwa na kampuni hiyo.
Alidai kuwa siku hiyo hiyo, maofisa wa TRA walitembelea eneo hilo kwa ajili ya ukaguzi wa kodi na kugundua kwamba walikwepa kodi kwa makusudi kwa kujifanya wamepokea fedha hizo kutoka kwa mteja, badala ya 550,000 alizokuwa amelipa.
Pia ilidaiwa baada ya ukaguzi, iligundulika kwamba sehemu ya mauzo ya nguo ambayo ni Sh 350,000 hazikuingizwa kwenye risiti hiyo ya EFDs. “Kutokana na uvunjifu wa sheria ya kodi, mshitakiwa wa kwanza na wa pili walipelekwa Kituo cha Polisi Stakishari na kuchukuliwa maelezo,” alidai Busegano.
Hata hivyo, Hakimu Hassan aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 9 mwaka huu itakapotajwa. Pia aliamuru kutolewa kwa hati ya kumkamata mshitakiwa wa nne, ambaye hakufika mahakamani hapo. Aidha, washitakiwa hao walilipa faini hiyo kukwepa adhabu ya jela.
Chanzo: Habari Leo