mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,735
Pamoja na Mikwara yote inayoendelea mipango ya Trump kufanya ambacho wenzake wameshindwa inakutana na Ukomo mapema sana.
ZIFUATAZO NDIO NJIA ZA AWALI KABLA YA VITA
1:Vikwazo vikali vipya vya Kiuchumi kwa N/Korea
N/Korea ndio nchi duniani yenye vikwazo vingi lakni bado imekuwa na Uwezo wa kutengeneza silaha hatari.
Sasa Trump kuwakomesha anafikiria kuzuia ndege zao zote kutokwenda mataifa mengine, Kuzuia mafuta kuingia nchni humo, Kuzizuia meli zake kutokukatiza bahari yoyote Ile, na Kuziadhibu na kuzikataza bank zote za China kufanya biashara na N/Korea (hapo pagumu)
2:Mashambulizi ya Virus kweny mitandao yote ya kijeshi Kwa kushirikiana na Israel
Anatarajia kufanya Israel walichowafanyia iran kwa kuwaingizia kirus hatari Stuxnet kuharibu mtambo ya Nuclear. Jaribio hili tayari US wamekwishafeli kila walipojaribu. Ikumbukwe N/Korea kikosi kinachopendwa na kulipwa mshahara mkubwa na marupurupu mengi ni kikosi cha jeshi la mtandao. Huko wamejidhatiti vilivyo na wanamitandao yao tofauti na hii ya kawaida. Kikosi Chao maarufu kama Bureau 121.
Kuna sintofahamu mbili wapo wanasema kufeli kwa Jaribio juzi ni matokeo ya shambulizi la mtandao kutoka US, wengine wanasema wao wenyewe walifanya makusudi ili tu kumuonyesha Trump japo hawakua na Nia ila wamefanya kile ambacho Trump alipaswa kujibu kijeshi lkn hadi sasa mzee Trump yuko kimya.
Inasemekana US wako katika mradi wa kutengeneza mfumo wa kuyahujumu mabomu ya masafa marefu ya adui zake kabla au wakati wa kuruhusiwa shambulizi badala ya kufunga mamitambo ya kukinga makombora.
3:Njia ya Tatu ni Mazungumzo
Miaka Saba Sasa toka mazungumzo Kati ya US na N/Korea yamefeli, njia hii hajawahi kusemwa waziwazi na Trump anaonekana kutoipa kipaumbele lakn wachina ndio wanaipendekeza zaidi kwa US.
4:Utata wa Kuivamia Kijeshi na kuifanya njia hii kuwa ngumu kwa US
Njia hii ni tata na inalenga kwanza kuzuia bahari Kim asifanye Jaribio la kombora lolote. Pili Kumpindua kabisa kijana Kim na kuukomesha utawala wake.
Tatizo haijulikani hawa N/Korea watajibu vipi hata kwa shambulio dogo tu kutoka US maana tayari wameshasema watashambulia kwa nguvu zao zote. Shambulio lolote lile linawaweka katika hatari raia zaid ya Mil 20 wa Korea kusini ambao wako ndani ya Range ya mabomu na vifaa lukuki vya kijeshi vilivyopangwa kwa ustadi mpakani vikisubiri amri. Wanatishia hadi kuisambaratisha ikulu ya S/Korea.
Ndio maana mshauri wa ulinzi wa Trump anasema nguvu ya kijeshi ni ya mwisho kabisa...
MAREJEREO
Factbox: Despite tough talk on North Korea, Trump's options limited