Wabunge wasiokaa kwenye majimbo yao

Wabunge wasiokaa kwenye majimbo yao

mfianchi

Platinum Member
Joined
Jul 1, 2009
Posts
11,925
Reaction score
8,444
Wandugu,wakati wa uchaguzi wa Igunga,tulisikia kuwa aliyekuwa mbunge wa hilo jimbo hakuwa na hata nyumba huko na wala alikuwa haishi jimboni mwake,naamini si yeye peke yake,mbali ya wabunge ambao ni mawaziri au wakuu wa mikoa ambao imebidi wakae mbali na majimbo yao(vituo vya kazi)naomba tuorodhesha majina yao hapa kuwakumbusha wajibu wao kuwa wanatakiwa wawe majimboni mwao na si Dar ambako wamefanya makazi yao ,naamini humu JF wamo ,na pia naamini kwa kuwaorodhesha hapa tutakuwa tumewakumbusha wajibu wao kwa wanachi waliowachagua na si vyama vilivyowateua ,nawakilisha
 
Kumekuwa na tabia ya wabunge, hasa wa majimbo ya pembezoni kukimbilia Dar es Salaam badala ya kukaa na wananchi wao ili watatue kero. Hatukatai wawepo Dar, lakini iwe kwa sababu maalum kama vile kufuatilia mambo wizarani na kuonana na viongozi wa ngazi za juu ambao wengi wapo Dar. Tukiondoa wale wa Dar na mawaziri, sema mbunge (jimbo lake) ambaye anaishi jimboni mwake na yule asiyeishi jimboni kwake na badala yake amekimbilia Dar na kurudi mara moja moja jimboni mwake hasa pakiwa na vuguvugu la kisiasa. Ikiwezekana mutoe na anuani ya makazi yake. Kazi ni kwenu wenye nchi!
 
Asumpta Mshama mbunge wa Nkenge mkoani Kagera yeye kaolewa Dodoma na anaishi hukohuko
 
Hapo hayamonia imefanya kazi lkn huyu mama wanaishi dom na mumewe ingawa alizaliwa bk na mumewe ni mtu wa Dom

Ok basi itakua ni ndoa ya pili maana watoto wale kuna teacher wangu ni muhaya na wanamuita shangazi
 
Waleta mada mmetuwekea vichekesho! Bora kutaja wabunge walioamua kuweka makazi majimboni mwao kuliko walio nje ya majimbo kwani hawa ni wengi karibia theruthi mbili wako nje ya majimbo yao; na hata wengine wako nje ya nchi kama Leticia Nyerere ambaye huishi uingereza na kuja bongo kula posho wakati wa vikao vya bunge. Hawa wabunge wote karibia wana majumba Dar na hata wakiwa majimboni shuguli zao zote na zinakuwa Dar.
 
Mwigulu na Lusinde wako bize kuinusuru chama.lazima wapigwe chini mana hamna maendeleo majimboni mwao
 
Mohamed Dewji,mbunge wa SINGIDA MJINI hakai jimboni.Yeye hata wakati wa vikao vya bunge Dodoma ukimpata huko nisawa na kuona KAKAKUONA.Naskia maranyingi anakuwa Marekani,Dubai,Uingereza kwenye biashara zake.
 
Dah Abood (M)morogoro mjini anajitahid kwenye jimbo lake.jamaa yuko bize na raia wake

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Mohamed Dewji,mbunge wa SINGIDA MJINI hakai jimboni.Yeye hata wakati wa vikao vya bunge Dodoma ukimpata huko nisawa na kuona KAKAKUONA.Naskia maranyingi anakuwa Marekani,Dubai,Uingereza kwenye biashara zake.

Still yet mnamchagua akiwapa unga
 
Back
Top Bottom