Wabunge waagiza fedha za maafa zikaguliwe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Cheyo(17).jpg

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC),John Cheyo


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema matumizi ya fedha za misaada zinazotolewa kupitia kitengo cha maafa hayaeleweki na kuagiza kufanyika ukaguzi wake kuanzia tukio la milipuko ya mabomu ya Mbagala, Gongo la Mboto pamoja na mafuriko ya mvua yaliyowakumba watu wa mabondeni mwishoni mwa mwaka jana.

Kamati hiyo pia imetaka fedha zinazotumika katika sherehe mbalimbali za kitaifa kuangaliwa ili wananchi wajue zilivyotumika
Hayo yalibainika jana baada ya PAC chini ya Mwenyekiti wake, John Cheyo, kupitia mahesabu ya kitengo hicho kilichopo Ofisi ya Waziri Mkuu.

Cheyo alitaka ukaguzi huo ufanywe na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ili kupata usahihi wa matumizi wa fedha hizo ambazo zimekuwa zikitolewa kila yanapotokea maafa.
Alitoa mfano kwamba serikali inasema imetoa magodoro

kwa watu waliokumbwa na maafa, lakini haisemi thamani yake ni kiasi gani hatua amabayo inaacha maswali mengi kwa wananchi.
“Ni vyema misaada hii ikawekwa wazi kuanzia ile ya mabomu ya Mbagala, Gongo la Mboto pamoja na mafuriko

ambayo yamliwakumba watu wa mabondeni,” alisema.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo, alipendekeza kitengo cha maafa kipatiwe hadhi ya kuwa Mamlaka ili kiweze kufanya kazi yake vizuri zaidi.Alisema kitengo cha maafa

kinakabiliwa na uhaba wa vifaa vya uokoaji kwa ajili kuwasaidia wananchi wanapopatwa na maafa ili kunusuru maisha na mali zao.
Lyimo alihojiwa na kamati hiyo ambapo alijibu maswali ya wajumbe ambao walitaka kujua shughuli za kitengo hicho ambacho.

Kuhusu hesabu za fedha za sherehe, Lyimo alishindwa kuzitolea maelezo na kuomba apewe muda na kudai kwamba mambo mengine hayatakiwa kufahamika kwenye vyombo vya habari.
Naye Mpigachapa Mkuu wa Serikali, Chobogoyo Kassian,

aliomba kamati hiyo isaidie ili bajeti ijayo aweze kupata Sh. bilioni tatu kununua mitambo mipya itakayosaidia kuchapisha nyaraka za serikali kwa wakati.
Alisema mwaka 2009 serikali ilinunua mitambo ya kwa kiasi cha Sh. bilioni saba, lakini imeshindwa kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa.


CHANZO: NIPASHE

 
Back
Top Bottom