Wabunge wa upinzani washirikishwe zoezi la ugawaji kitambulisho cha mjasiriamali hasa mkoa wa Iringa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,959
141,956
Huu ni ushauri tu kwani maendeleo hayana chama.

Nipo hapa miyomboni katika manispaa ya Iringa na nilichoshuhudia ni kwamba elimu ya kitambulisho cha mjasiriamali haijaeleweka kabisa hapa.
Na inawezekana Kasesela na Happi bado hawajawaelewa vilivyo wakazi wa mkoa huu, yaani wanawaelewa kiofisi zaidi kuliko kimtaa.

Niwashauri tu viongozi hawa wamshirikishe mbunge na madiwani katika zoezi hili vinginevyo sitashangaa yakiwakuta yale ya Makalla wa katavi.

Navalonge swela
Maendeleo hayana vyama!
 
Kweli maendeleo hayana chama ila cha kujivunia nasikia magu kaendesha kikao kwa kiinglish huko Namibia
 
wahehe vitambulisho vya elfu 20 tu wameshindwa kununua wanachojua ni kunywa ulanzi tu. wasiwalazimishe wanaweza wakajinyonga
 
wahehe vitambulisho vya elfu 20 tu wameshindwa kununua wanachojua ni kunywa ulanzi tu. wasiwalazimishe wanaweza wakajinyonga
Hahahaa .......kule kwenu ukingani Ole Sendeka kauza vitambulisho 6000 tu kati ya 60,000 sawasawa na 10%.
Afadhali ya Happi kauza 16000!

Maendeleo hayana vyama!
 
Huu ni ushauri tu kwani maendeleo hayana chama.

Nipo hapa miyomboni katika manispaa ya Iringa na nilichoshuhudia ni kwamba elimu ya kitambulisho cha mjasiriamali haijaeleweka kabisa hapa.
Na inawezekana Kasesela na Happi bado hawajawaelewa vilivyo wakazi wa mkoa huu, yaani wanawaelewa kiofisi zaidi kuliko kimtaa.

Niwashauri tu viongozi hawa wamshirikishe mbunge na madiwani katika zoezi hili vinginevyo sitashangaa yakiwakuta yale ya Makalla wa katavi.

Navalonge swela
Maendeleo hayana vyama!
Tatizo hao ni vifutu wanachojua wao ni kujifutua tu.
 
Kweli maendeleo hayana chama ila cha kujivunia nasikia magu kaendesha kikao kwa kiinglish huko Namibia

Hapo ndio mzee baba akiteleza na ung'eng'e huko Namibia.
Habari hii itaandikwa na gazeti LA Uhuru na Tanzanite kwa majuma kadhaa kumuenzi.
"Maendeleo hayana lugha"
 
Yaani umwambie mheshimiwa Msingwa ashiriki failure plan kama hii ya vitambulisho?
Hamumpati ng'oo!
 
Napinga hoja yako vibaya sana ! hilo gunia la misumali walibebe wenyewe , ubabe utasababisha mtu mwingine aamkie makaburi ya Kihesa
 
Kwani wanavigawa au wanaviuza?! Kama vinauzwa, Nashauri wavinunue wao viongozi, mkuu wa mkoa na wakuu wawilaya, kisha wavigawe kwa hao wananchi, hii haitachukua muda kuvimaliza.
 
Kwani wanavigawa au wanaviuza?! Kama vinauzwa, Nashauri wavinunue wao viongozi, mkuu wa mkoa na wakuu wawilaya, kisha wavigawe kwa hao wananchi, hii haitachukua muda kuvimaliza.
Hata mbunge alipaswa kuvinunua ili awagawie wapiga kura wake!
 
...Na inawezekana Kasesela na Happi bado hawajawaelewa vilivyo wakazi wa mkoa huu, yaani wanawaelewa kiofisi zaidi kuliko kimtaa....
Maandamano.jpg

Nashauri zoezi libadilike kwa wenzetu WAHEHE kila ukinunua kitambulisho unaondoka na the dog mmoja!
 
Back
Top Bottom