Tetesi: Wabunge wa Upinzani na kujirekodi sauti

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
"Naamini umenisikia ingawa hujaniona, au!" Ndivyo Wabunge wetu Waheshimiwa wanataka iwe. Huo ndo uwakilishi wao uliotukuka. Soma hii hapa chini:
"Wabunge wa upinzani wameibuka na mbinu mpya ya kujirekodi wenyewe sauti kwa kutumia simu, wakati wakitoa michango yao bungeni kisha kutuma michango hiyo kwenye mitandao ya kijamii kama WhatsApp na redio zilizo majimboni mwao. Hatua hiyo imetokana na Bunge kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya televisheni na redio".

Je, unawaunga mkono wabunge wa upinzani kwa mbinu hii au unawapinga? (Nukuu toka facebook)
 
tuko na kalam zenye camera 6.7 na wi-fi na zinarusha live

swissme
 
tuko na kalam zenye camera 6.7 na wi-fi na zinarusha live

swissme

Aluu, hongereni! Mko juu! Wasaidieni wananchi jimboni kwenu kuwa juu kama nyie kwa vitendo. Mtapendwa na hata kubebwa kuliko uvuvuzela kwenye mjengo. Japo unapotoka mjengoni urudi jimboni kuendeleza uvuvuzela huo kwa njia nyingine km kuhamasisha. Naamini watakurudisha mjengoni 2020. Mh Mbatia juzi katembelea eneo lililokumbwa na maporomoko ya mvua na kuwaasa wananchi wake akioneshwa kwenye TV. Huo ndo wajibu wa Mbunge yeyote. Dole juu Mh Mbatia.
 
pumba tupu.

swissme
 
Nimemsikia Zitto na Lema,..kiukweli tunaitaji waponzan imara kama walivyo sasa
 
Back
Top Bottom