crome20
JF-Expert Member
- Feb 5, 2010
- 1,168
- 779
Nimekuwa nikifuatilia hoja za Wabunge wa CCM kupinga kukatwa kodi kwenye kiinua mgongo chao, bado sijapata hoja yenye mashiko.
Na Je serikali ya CCM itasalimu amri mbele ya wabunge wake? Karibu tujadili
- Wapo wanosema kwa kipindi chote cha miaka mitano wanakuwa wakilipa kodi kwenye mishahara yao hivyo sio sahihi kiinua mgongo kukatwa kodi. Hapa Napata tabu na hoja hii, kwani hata watumishi wengine ambao kiinua mgongo chao kimekuwa kinakatwa kodi, wanalipa PAYE kila mwezi na hivyo kuifanya hoja hiyo niione haina mashiko.
- Wapo wanosema pesa wanazopata sehemu kubwa inaishia jimboni kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi na kwamba wabunge wamegeuzwa ATM huko vijijini. Mimi napinga hoja hii kwani kazi ya mbunge si kutoa michango ya pesa, mbunge mahili ni yule anayetumia maarifa na ubunifu kuzalisha ajira na kupunguza tabia ya kuombaomba. Sio wabunge tu wnaoombwa pesa, hata watumishi na wafanyabiashara mbalimbali hali hiyo inawapata hivyo hiyo sio hoja kabisa. Na zaidi ikumbukwe kuwa kodi inayokatwa itaenda kutoa huduma za jamii hiyo hiyo ambayo wanajinasibu kuisadia, hapo halija haribika neno.
- Wapo wanosema kwa nini Viongozi wakuu wengine kama Rais, Majaji n.k wao hawakatwi bali iwe kwao tu. Mimi nadhani hoja hapa si kupinga kukatwa bali kukubali na kuongeza kada zingine ambazo nazo zinatakiwa kukatwa kodi kwenye kiinua mgongo kama ilivyo kwa watumishi wote. Kutokushitakiwa kwa mtenda kosa A hakumfanyi mtenda kosa B aachiwe huru.
Na Je serikali ya CCM itasalimu amri mbele ya wabunge wake? Karibu tujadili