wabunge wa CCM bwana!

wabunge wa CCM bwana!

tufe

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2015
Posts
750
Reaction score
290
Wanajamii,

Kuna wakati wabunge wa CCM huwa wananipa wakati mgumu kweli kuwaelewa. Utamkuta mbunge wa CCM anasimama bungeni na kuongea kana kwamba yeye ni mjumbe wa baraza la mawaziri. Sasa mimi huniacha hoi na kubaki kujiuliza hivi hawa wabunge wa CCM hawajui kazi na wajibu wa mbunge anapokuwa bungeni? Hivi wao hawajui kwamba pamoja na majukumu mengine, majukumu ya mbunge ni kuisimamia,kuishauri,kuikosoa na kuiwajibisha serikali? Ni kweli katika mabunge ya kunakuwa na kambi mbili. Kambi ya upinzani na kambi ya chama tawala. Lakini kuwa kambi ya chama tawala hakumuondoshei mbunge wajibu wake mkuu wa kisheria. Inafika mahali katika bunge letu haujui Waziri ni nani na mbunge ni nani Wote wamegeuka wasemaji wa serikali. Sasa katika hali kama hiyo bunge linamaana linamaana gani? Yanini kupoteza pesa za wavuja jasho masikini wa nchi hii?
 
Kweli umenena mkuu hawajui majukumu yao km wabunge.hukumu yao ni october tupa kule maccm
 
Hakika mkuu hawa dawa yao ni October tu.
 
Sambaza elimu ya uraia tuwafute kazi October!!
 
Wabunge wa ccm wa hovyo sana,wenzetu hujadili mambo ya teknolojia,uchumi na vitu vya msingi wao hoja yao ndo zile za kina lusinde kwamba ""kama Dr slaa ana nguvu mleteni yule mzee nikimpiga ngumi moja naua"
 
Hii ndio shida ya kuchagua wabunge waliokufa akili na walio na msongo wa mawazo juu ya kupoteza majimbo yao.
 
Mimi siwalaumu sana ccm na mibunge yao, ila akili za watanzania sijui nani aliyeturoga tunaona watu wanavyoboronga bungeni lakini tunawarudisha hao hao tena, 2015 ccm wakishinda kwa kishindo kama wanavyojitapa itabidi ushauri wa Mkosamali ufanyiwe upembuzi yakinifu tutafute consultancy wa kutupima akili. Naichukia ccm na mambo yake yote toka sakafu ya moyo wangu na hawawezi kurekebika unless watoke madarakani na wafe natural death iliyokufa KANU, ila najipa moyo maana naamini ipo siku chama hiki kitaondoka, ninaomba Maulana aniweke hai nije kushuhudia hyo siku njema, CCM wamejigeuza kama Mkimwa kwa wale walosoma tamthilia ya Shamba la Wanyama (Animals Farm by George Orwell).
 
Wanajamii,

Kuna wakati wabunge wa CCM huwa wananipa wakati mgumu kweli kuwaelewa. Utamkuta mbunge wa CCM anasimama bungeni na kuongea kana kwamba yeye ni mjumbe wa baraza la mawaziri. Sasa mimi huniacha hoi na kubaki kujiuliza hivi hawa wabunge wa CCM hawajui kazi na wajibu wa mbunge anapokuwa bungeni? Hivi wao hawajui kwamba pamoja na majukumu mengine, majukumu ya mbunge ni kuisimamia,kuishauri,kuikosoa na kuiwajibisha serikali? Ni kweli katika mabunge ya kunakuwa na kambi mbili. Kambi ya upinzani na kambi ya chama tawala. Lakini kuwa kambi ya chama tawala hakumuondoshei mbunge wajibu wake mkuu wa kisheria. Inafika mahali katika bunge letu haujui Waziri ni nani na mbunge ni nani Wote wamegeuka wasemaji wa serikali. Sasa katika hali kama hiyo bunge linamaana linamaana gani? Yanini kupoteza pesa za wavuja jasho masikini wa nchi hii?

Yaan mkubwa me pia najiuliza sana swali hili yaan huwezi tofautisha waziri na mmbunge wote wanaitetea serikali kusema kweli ccm no janga la taifa hili na ccm ni zaidi ya mzimu
 
Back
Top Bottom