Wabunge Vijana Wanaharibu hadhi ya Bunge

Njanga Tz

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
843
654
Kwa kiasi kikubwa nilitegemea uwepo wa vijana wengi katika bunge la 11 ingekua chachu ya kuibua hoja zenye akili lakini mpaka sasa hakuna matumaini labda tuendelee kusubiri.

Ninachoshuhudia ni wabunge vijana kuendeshwa na mihemko,kutaka sifa na kujifanya wajuaji hasa waliorudi kwa muhula wa pili.

Wengi wao hawajui kuongea vizur,kwa heshima wala kwa nidhamu.Wanaongea ovyo kwa lugha zisizo na hadhi ya Bunge.
Mfano ni maneno ya J. Mbilinyi na wengine.

Ni vijana wanaopenda kubishana na kuleta vurugu kwa wazee wao mfano ni Mama Kafulila, Halima mdee na Dr Mwakyembe,Tulia na Ma Sita.

Wengi ni wapenda sifa mfano Lusinde,Said kubenea,Tundu Lisu, Kigwangala na Zito Kabwe.

Kama hili Bunge litaendelea na vihoja hivihvi ni bora tukawarudisha wazee wetu wakina Sita, Mwandosya, Dr Slaa na wengne ili tupunguze vijana bungeni.

Mwisho tunawataka Wabunge Vijana wawe na nidhamu,heshima, uadilifu kwenye kuongea ili Bunge libaki na hadhi yake.

# WABUNGE VIJANA PUNGUZENI MIZUKA
 
hao wametumwa sasa hawana hoja kwa serikali wanaparamia hovyo.pamoja na yote hayo Mwakyembe lazima atasimamia ianzishwe mahakama ya ufisadi naye anaushahidi tosha kuhusu richmond
 
Tatizo huku vijiweni ili uongelewe lazima uwe umebwata sana hapo bungeni...hata kama kubwata huko ulikuwa unaongelea shanga badala ya maji
Shanga na maji vyote vina umuhimu wake. Bila shanga hayo maji nani angekuwa na shida nayo? Shida ya elimu yetu ni ukariri!
 
Huyu mleta mada amewakumbuka wakina cheyo, mrema, wasira, veridiana mg'ong'o na wengine wa aina hiyo
 
Imekaa kubomoa zaidi..kama ambavyo mlivyo aminishwa kua Chadema ni uchaga na ukabila na udini.
Ukiwa mmlumumba akili huwa ni moja tu..muwe mnachanganya na zenu
 
Kama Mwakyembe ataanzisha Mahakama ya mafisadi inabidi awe wa kwanza kuhukumiwa kwa kununua mabehewa fake.
 
Imekaa kubomoa zaidi..kama ambavyo mlivyo aminishwa kua Chadema ni uchaga na ukabila na udini.
Ukiwa mmlumumba akili huwa ni moja tu..muwe mnachanganya na zenu
Halafu jaribu basi kutueleza muelekeo wa wabunge vijana bungeni km hutaishia na neno wanataka sifa za kijinga.
 
Back
Top Bottom