Wabunge ongeeni.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,209
4,406
WABUNGE ONGEENI.


1)Wangu wosi pokeeni,taratibu chukueni
Sitaki kuwakwazeni,ila kitu wambieni.
Muwe macho mjengoni,kulalala chukieni
Na wabunge ongeeni,mkishindwa piganeni.




2)wasije nyamazisheni,kimya kuja nyamazeni
Nanyi kimya tulieni,tulyeni kama foleni.
Mchekwe mpo jengoni.
Na wabunge ongeeni,mkishindwa piganeni.



3)sheria zenu kichwani,msije zacha garini.
Garilo la mkoponi,lidaiwe msakoni.
Muswada muwe makini,na muswala weka chini.
Na wabunge ongeeni,mkishindwa piganeni



4)kugoma goma gomeni,mkichoka wasuteni.
Kutoka toka tokeni,katu msiogopeni.
Na wabunge ongeeni,mkishindwa piganeni.



5)simanishi kunjaneni,namanisha ongeeni.
Sana sana msemeni , ikibidi msuseni.
Namaanisha shindeni,na kwa hoja onganeni.
Na wabunge ongeeni,mkishindwa piganeni.


Shairi=WABUNGE ONGEENI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom