wabunge kupoteza nafasi zao

marveljt

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
1,503
1,479
Hadi kufikia 2020 baada ya uchaguzi mkuu idadi kubwa ya wabunge walioko hawatakuwepo kwenye nafasi zao. Hii ni kutokana na mienendo ya muda huu ilivyo.
Kwa chama cha ccm wengi wao wataondolewa na uongozi kwa vigezo tofauti k.m kutokuwajibika ipasavyo,kutokufuata taratibu za chama,kutokuitetea serikali na badala yake wale wabunge walioteuliwa sasa hivi na baadhi ya viongozi walioko katika nyadhifa mbalimbali utakuwa ndiyo muda wao wa kugombea katika maeneo waliyotoka.

Kwa upinzani nako mambo ndiyo mabaya zaidi. Kwanza kuna makundi ya viongozi na pia kuna wananchi. Katika vyama vya upinzani viongozi wakuu( katibu,mwenyekiti) wana watu wao ambao ndiyo watakaopewa kipaumbele katika uchukuaji wa fomu. Kwa wale watakaoachwa kuendelea watakutana na kizuizi kingine mbele ya wananchi. Kadri muda unavyoendelea sasa hivi wananchi wanaangalia mahali walipokosea na ni jukumu la wabunge walioko madarakani muda huu kurekebisha pale wanapoweza. Maendeleo huletwa na mwananchi chini ya usimamizi wa serikali. Mf. Kwa sasa wapinzani wanalalamika wamezuiwa kufanya mikutano hiyo siyo hoja kubwa kwani kwa hao waliochaguliwa wanafaa sana kuwa chachu ya mabadiliko kwa sehemu zingine. Ni muda wao muafaka wakuwa karibu na wananchi na kutatua kero ndogo ndogo na hivyo wananchi kujua kuwa mbunge,diwani,mwenyekiti yuko na sisi na anatujali. Upinzani ukisema usubiri hadi mwaka 2019 waanze kupambana na ccm watakuwa wanapoteza muda kwani huo ndiyo muda ambao miradi itasambaa ili kuwazubaisha wananchi nankusahau kabisa upinzani.

Wabunge wa upinzani mnatakiwa kuonyesha njia kwa wananchi wa maeneo mengine na siyo kupiga taarabu kama ccm.watanzania wanasafiri kila leo hivyo ni rahisi kutoa picha mbaya/nzuri sehemu moja kwenda nyingine. Wakati ni huu
 
Back
Top Bottom