Wabunge CCM janga la Taifa

Wabunge CCM janga la Taifa

Dennis Tesha

Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
16
Reaction score
23
Nikiwa kama kijana wa kitanzania mwenye umri mdogo sana, Napata mashaka makubwa sana na viongozi wa Taifa langu hili;
Kama kweli ni kwamba wanauchungu na maisha ya mwananchi wa nchi hii?
Na kama kweli wanauzalendo wakutetea rasilimali za nchi hii?
Na kama kweli wananidhamu na matumizi ya kodi za wavuja jasho wa nchi hii?
Na kama kweli wanao uwezo wakukusanya kodi kama inavyostahili.

Nikijiuliza hayo machache tu, fikra zangu zinakutana na dudu linaitwa ESCROW ambalo hakika kwa sasa limeitafuna bila shaka kila fikra za Mtanzania, kwani linapita kila kona ya nchi hii na hakuna namna ambayo masikio yetu hayakupitiwa na dudu hili.

Jana kamati ya PAC chini ya mwenyekiti wake Zitto Kabwe iliweza kwa kiasi kikubwa na kwa uzalendo mkubwa kulielezea vyema hili dudu lililotafuna fedha za wavujajasho watanzania na kuwanufaisha kibinafsi baadhi ya viongozi wa nchi hii, kupitia mihuri ya viongozi hao hao kuweza kula fedha hizo kwa njia sisizo halali. Na kwa bahati mbaya pia hata Askofu wa kanisa langu nililo na imani yake kapata mgao kitu ambacho kinanisikitisha sana.

Sasa basi baada ya ripoti ya PAC kuanika madudu ya dudu hilo, leo ndiyo nimezidi kupata mashaka na viongozi wa nchi hii hasa wabunge wanaotokana na CCM kwa michango yao bungeni isiyokuwa na uchungu na Taifa hili, kwa kuipinga waziwazi ripoti ya kamati ya PAC na mapendezo yake iliyo yatoa kwabunge, nakusahau kamati hiyo ilisheheni wajumbe wanaotokana na chama chao(19) na wapinzani(5) pekee. Jumla kuwa 24.

Nazitafakari hizi bilioni(321) ambazo wamezipigia kelele kwamba siyo fedha za umma, na kutazama mammlaka kama TAKUKURU, na Ofisi ya CGA ambazo zilichunguza na kubainisha dudu hili ESCROW limekula fedha za umma kupitia mifuko binafsi ya viongozi na kuthibitishwa na PAC, wabunge hawa wa CCM wanatoka jasho kweli kweli kutetea serekali yao ndani ya bunge huku wakiwa na hoja hafifu kama Mh.Mariam Kisangi, Mh.Livingstone Lusinde(Mipasho) Mh.Richard Ndassa na wengine waliochangia jioni ya leo ili mapendekezo ya PAC yasifanyiwekazi kwa kuwawajibisha waliohusika.

Heshima kwenu wazalendo wa kweli Mh. Tundu Lissu, Mh. David Kafulila na kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni(KUB) Mh.Freeman Mbowe kwa michango iliyoonyesha uchungu mkubwa na upotoshaji uliofanywa na Prof. Sospeter Muhongo na wabunge wa CCM waliochangia kuwa fedha za ESCROW hazikuwa za umma.

Ila niwape pole wabunge wa CCM na washirika wao kuwa watanzania walichokisika jana tarehe 26 Nov 2014 kutoka kwenye ripoti ya kamati ya PAC iliyowasilishwa bungeni juu ya sakata la dudu ESCROW nivigumu kufutika kwenye fikra zao kwa waliyosikia na ningumu kuwa na imani nao tena na ndiyo anguko lao na siku zao zinahesabika watakavyofunika kombe mwanaharamu dudu ESCROW apite.
 
ndasa amalizie mda wake hatumtaki tena sumve, hicho ndo tulikutuma bungen ukawateteee wezi wa mali za umma? umenikera sana mzee wangi naona huu ndo mwisho wako
 
Huyu Mbunge wa Magomeni Chomboh eti naye Mbunge. Jamani tuna Wabunge.
 
Wabunge wa CCM mnawaonea BURE. Wataalamu wa mambo ya sosholoji wanasema, ''Kila jamii hupata viongozi inaowastahili''. Jamii ikiwa ya watu makini hupata viongozi makini, jamii ya watu hovyo hupata viongozi wa hovyo.
Kama watu hawataki kupiga kula na wale wanaopiga kula wanahongeka kwanini viongozi wetu wasiwe mfano wa hao wanaoongea mipasho badala ya kutoa michango thabiti.
 
Yaani wamenifanya niipende siasa. 2015 nitakwenda kumuondoa mbunge mmoja wa ccm. Vijana twendeni tuwaondoe wabunge wote wajinga wajinga
 
Back
Top Bottom