Wabongo tunafeli wapi kwenye pricing and location?

Bei za bidhaa za mitandaoni pasua kichwa kwakweli, hazina uhalisia kabisa.
 
Matapeli hao.
Walitaka kuniibia milioni 2 wakidai nikishalipa wananiletea tv mpaka mlangoni.
 
Msichojua ni kwamba,
1. Instagram na social media nyingi si wauzaji wenyewe ila ni madalali. Na unajua dalali ni lazima amsome mteja kabla ya kumpa bei.
2. TRA wanachukulia bei uiliyoitaja kikupigia kodi ya kulipa. TRA ni mzigo mzito. Wamefika mahali wanachukua bei kutoka amazon, alibaba ili kukupiga kodi.

3. Mteja wa kweli ataenda DM au whatsap na biashara kufanyika
 
Kuna situation nimekutana nayo kwa madalali wa magari mpaka inastaajabisha.

Gari moja (namba ya usajili ni ileile) ila kila dalali anaitangaza kwa specs tofauti tofauti.

Mmoja 70,000Km mwingine 45,000Km

Mmoja ya mwaka 2009 mwingine 2010 mwingine 2008.

Mwingine 1.5L mwingine 1.8L mwingine 2.0L ila gari moja.

Huyu iko Dar,yule Dodoma na huyu iko Mwanza.

Kuna mpaka Premio na Allion za 1290cc huko au 7 seats na mtu karudia tangazo hilo kwa gari nne tofauti.
 
Changamoto nyingine yakuweka bei watatokea chuki binafsi na kuanza kuiponda bei na hata sio wanunuzi kwahiyo unakuta gafla comment 200 zote ni udaku hili pia ni tatizo jingine
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…