Waasisi wa CCM wametufikisha hapa tulipo

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,423
13,935
Viongozi wetu waliopita walihakikisha kuwa CCM inashinda na kutawala jua liwake au mvua inyeshe bila kuzingatia wananchi wanasemaje, wanataka nini na wana hali gani. Hata Katiba ya nchi iliandikwa kwa kuihakikishia CCM kutawala milele. Lakini hawakuwa na maono kuhusu tabia yao hiyo kwa siku za mbeleni kama akijatokea mtawala asiyependa demokrasia na asiyekuwa na maadali. Hawakujua kuwa walitengeza robot ambalo lingewezakuja kuivuruga nchi na hata kuwavuruga hata wao wenyewe kwa wenyewe siku za mbeleni. Tumeona namna robot lao lilivyo mkumba mzee Warioba, Kingunge, Sumaye, Lowassa, Moyo, na wengine wengi walioshiriki kuliunda robot. Tumeliona robot lilivyokumba nyumba za serikali, viwanda, mashirika ya umma, madini yetu. Robot limeikumba sekta ya ajira na elimu kwakusababisha watumishi na wanafunzi hewa, wizi, ufisadi, na ukwepaji kodi. Hivi Sasa hatujui robot lao litakumba nini, nani na vitu gani kesho na keshokutwa.
 
Back
Top Bottom