Waajiriwa acheni kuishi kwa presha

Greg50

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
1,953
2,431
Nanukuu

"Nimeona hivi karibuni kila mwajiriwa akijaribu kusave hela na kukopa ili kuanzisha kabiashara flani au mradi kwa lengo la kuja kuacha kazi.

Nadhani hii inasababishwa na maneno ya motivational speakers kuwa hakuna tajiri alieajiriwa bali wote wamejiajiri. Lakini biashara hizi nyingi zimekua zikifa kifo cha mende au hata ikifanikiwa basi ni faida ndogo sana.

Sasa kuna haja gani ya kuishi kwa presha na kujibana usipate hata serengeti baridi weekend kisa tu biashara uchwara. Sio kila mtu lazima awe Dewji, nashauri tuu mjenge kamjengo ka kuishi, mmiliki ka ist kakali, kujiongeza elimu kwa lengo la kupandishwa cheo na kuwekeza miradi ya muda mrefu kama mashamba ya miti ili ukistaafu uweze kujihudumia mwenyewe bila kutegemea watoto"

Mwisho wa kunukuu. Jumamosi njema.
 
hakuna kitu kama
"kamjengo kakuishi" mjengo ni mjengo kweli, na hakuna ka ist kakali, ist itabaki kuwa ist tu
kufanya kazi yakuajiriwa kwa takaribani maisha yako yote huo ni ulemavu wa akili, mpango wa pepembeni (biashara) ni muhimu sana, ongeza kipato chako + ongeza maitaji yako, na kama michongo yapembeni ikisimama vizur unapiga chini tu ajira yako

"utumwa kwa muafrika ishakua kama sehemu ya utamaduni wake"
 
Kuwa employed sio utumwa mkuu
 
Nanukuu

"Nimeona hivi karibuni kila mwajiriwa akijaribu kusave hela na kukopa ili kuanzisha kabiashara flani au mradi kwa lengo la kuja kuacha kazi.

Nadhani hii inasababishwa na maneno ya motivational speakers kuwa hakuna tajiri alieajiriwa bali wote wamejiajiri. Lakini biashara hizi nyingi zimekua zikifa kifo cha mende au hata ikifanikiwa basi ni faida ndogo sana.

Sasa kuna haja gani ya kuishi kwa presha na kujibana usipate hata serengeti baridi weekend kisa tu biashara uchwara. Sio kila mtu lazima awe Dewji, nashauri tuu mjenge kamjengo ka kuishi, mmiliki ka ist kakali, kujiongeza elimu kwa lengo la kupandishwa cheo na kuwekeza miradi ya muda mrefu kama mashamba ya miti ili ukistaafu uweze kujihudumia mwenyewe bila kutegemea watoto"

Mwisho wa kunukuu. Jumamosi njema.
Sawa nimekupata isipokuwa hapo uliposema "kujipatia Serengeti baridi" badala yake ungesema "juice baridi" au "maziwa fresh"
 
Back
Top Bottom