Waafrika tulilogwa au ndo tulivyo? Inasikitisha kwa kweli

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Hii si mara ya kwanza na haitakuwa mara ya mwisho kuandika kuhusu uwezo wa kiakili wa waafrika wenzangu kwa sababu kwenye thread zangu zilizopita kama mbili au tatu nimelizungumzia hili suala kwa mapana sana kuhusu kuwa na hofu na doubt na akili ya mtu mweusi mwenzangu. Sitaki kueleza niliyowai kuyaandika nyuma ila nimeyaandika mengi sana huku nikiwa ninamnukuu dr watson moja ya mwanasayansi maarufu na bora zaidi duniani aliyewai kusema na hadi kuandika kitabu huku ndani yake akisema ana wasiwasi na akili ya mtu mweusi.

Leo nitazungumzia mada hii nikiwa naongelea gazeti la nipashe ambalo ni gazeti la mtanzania mwenzetu na lenye waandishi wa habari napenda kubashiri kuwa wengi wao ni watanzania.

Kwenye page ya mwanzo kabisa ya gazeti hili wamezungumzia kubaki siku kadhaa kufikia siku ya uchaguzi na kwenye vipengele vya habari iyo wakasema watanzania wenye asili ya kiasia wameanza kukimbia nchi. Tena imewekwa page ya mbele kabisa.

Kwenye mada kuu nimesema kama kuuliza kuwa je waafrika tulilogwa au ndo tulivo nikiwa ninamaanisha kwa akili ya mhariri wa nipashe na waandishi wake wameonesha ni kwa jinsi gani waafrika ni kuwa kama hatukulogwa kichwani basi tuna walakini kwa sababu hii habari wanaweza wakawa wameiandika either kwa kuuza gazeti au kwa kufanya gazeti lao litoe stori inayozungumzwa sana ila nauhakika hawa watu hawakupima impact ya habari husika katika usalama wa taifa na impact kwa taifa kimataifa hasa katika uchumi. Labda wakiwa na motive nyingine pembeni hapo sawa nitaelewa kuwa basi hawakukosea motive iyo ambayo obvious itakuwa evil motive.

Siku zote ikifika uchaguzi watu wa asili ya asia uwa wanaenda kwao na kurudi baada ya uchaguzi ila hata siku moja vyombo vya habari havikuwai kuandika huko nyuma, iweje leo gazeti la nipashe waitoe kama habari ya kwanza hasa kwenye uchaguzi huu ambao jamii imejengewa tension ambayo sio ya msingi na imeonekana kuwa inaweza kwenda kuharibu amani ya nchi na baadae kuharibu uchumi wa nchi??????

Kwa watu ambao hamjanielewa bado napenda kufafanua kuwa siku zote habari mbaya kuhusu nchi za kiafrika hasa kwenye kipindi cha uchaguzi ni vyombo vya habari vya magharibi na ulaya ndo vimekuwa zikizitangaza nchi za kiafrika vibaya tena mara nyingi ni either kwa kuzimaliza izo nchi kiuchumi kwa mfano pale cnn inapotangaza wageni waanza kukimbia tanzania basi dunia nzima itaogopa kuja tanzania na hatimaye tanzania itacollapse kiuchumi kwa kukosa wageni hasa watalii au kama sio ivo ni kuonyesha tu chuki zake na nchi za kiafrika. Sasa kilichonishangaza ni how comes gazeti la waafrika lililo afrika ndo linaandika habari hii ambayo kwa jicho la tatu imeleta tension kubwa sana kwa jamii ndani na nje na inaonekana italeta impact kubwa sana kwa taifa kiuchumi??????

Kusema ukweli gazeti la nipashe mmenisikitisha sana na napenda muende kenya tu mkajifunze umuhimu wa media za ndani kutoweka tension kwa jamii. Kwa sababu kenya nao media za magharibi walizitangaza vibaya sana na media za ndani zilifuata mkumbo huo ila walikuja kujifunza pale walipofeel impact ya yaliyowakuta hasa kiuchumi kitu kilichasababisha media za ndani kuanza kuitangaza vizuri nchi yao na hadi sasa hali ya kiuchumi imeanza kukaa sawa.

Nipashe kama mna evil motive na taifa hili napenda kuwakanya ila kama mliteleza mungu awarehemu.

Mungu ibariki tanzania na watanzania.

===================================

Chanzo: Nipashe
 
Thanks moderator kwa kuunganisha na habari husika. Tanzania kwanza vyama baadae.
 


Hata kidogo Mungu hawezi kutubariki wakati wewe hutaki kutumia akili yako. Wewe bado una yale mambo ya kikale ya kuita beleshi kijiko kikubwa. Umekiri ni ukweli hawa jamaa huwa wanaondoka, sasa huoni Nipashe wameripoti kitu cha ukweli? Kwanini unakuta mtu mwenye uraia wa Tanzania halafu eti akimbie wakati wa uchaguzi? Anaogopa nini?
 
Nafikiri hujaelewa mantiki ya mada husika. Nakushauri fuatilia tena na tena na ujifunze sana kuhusu siasa za dunia na mambo ya dunia ndugu alafu utaelewa nazungumzia nini.
Kwa kifupi kila jambo lina maana yake na umuhimu na ubaya wake kulingana na hali ya wakati husika. Kuna habari unapoitangaza tena kwa kuipa uzito kipindi fulani unaweza dhani kuwa umehabarisha kume ndo umezidi kujimaliza kwa kuongeza tension kwa wananchi na sio ivo tu bali ni pia kufanya nchi yako iathirike kiuchumi kutokana na wageni kuanza kuiogopa. Kama unabisha kawaulize kenya walijifunza nini kutokana na kuendekeza habari za ovyo zisizo na maana hasa kipindi kibaya ilivowaghalimu kiuchumi.
 
Siwezi kusema waafrika tumelogwa au tumelaaniwa, kwa kusema hivyo najiloga na kujilaani mwenyewe.

Waafrika hutenda au husema bila uoga kile wanachotaka tenda au kusema. Huwa sio wanafiki hata kidogo. Ktk hili inategemea uwezo wake kufikiri na kuona madhara ya kile anachokitenda au kukisema.
 

umekubali kwamba ni kweli wanye asili ya kiasia wanaondoka kwa hofu ya usalama wao ila unalalamika kwa magezeti kutokufanya hivyo huko nyuma,nafikiri sasa ungepongeza magazeti kwakujirekebisha na kuanza kutoa habari ambazo hapo mwanzo hawakufanya hivyo.
Utakua umerogwa peke yako usitujumuishe
 
Sio wote. Waafrika wengine wako vizur.
Lakini kwa wengine, Mwafrika kukumbukana mwisho wiki 1 nyuma. Hana kumbukumbu zaid ya hapo
Wengine, sio wasomaji wakubwa. Hata wasomi wetu husoma vitu vinavyo husu kazi wazifanyazo tu, na magazeti ya udaku. Kwahyo hana nafas ya kujipanua mawazo
Ukikuta a nachek TV itakuwa music

Majuz juzi hapa tumeambiawa watanzania tuna IQ ya chini zaid. Hilo si ajabu. Ndio weng wetu hao. Sasa ndio hao watakao mchagua rais wa Tanzania jpili ijayo. Mbona kazi!
 
Kwa sisi waafrika ungesema tu kwa kifupi ukiwianisha na mambo tunayoyapenda. Kwa mfano ungesema ukimkasilikia mkeo na ukamwambia kuwa "wewe mwanamke kila mwanamme unamkubali" kesho watajaa wageni wa kiume nyumbani kwako maana wengine huwa wanatafuta pa kujifunzia, si vyema sana kusema kila kitu hata kama ni kweli
 
Afrika hatujawahi kukubali demokrasia.

Tumelazimishwa na mataifa ya nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…