Waafrika tuijenge Afrika yetu.

Vumilika

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2017
Posts
2,306
Reaction score
2,688
Maamkizi mema, amani na upendo kwa kila mwenye kuisoma mada hii.
Ni imani yangu kubwa kuwa tupo salama na wenye afya njema. Kama kichwa cha habari kinavyosomeka kuna mambo mengi zaidi ya kujadili ili tuweze kufanikisha lengo hili. Kutokana na wimbi kubwa la waafrika kujaribu kukimbia nchi zao na kuhamia nchi nyingine kwa ajili ya hali ya kisiasa, kiuchumi, kimaendeleo na zinginezo, inatupasa tuangaliye wapi tunakosea ili tuweze kuparekebisha na waafrika tuweze kuishi kwa amani, upendo katika bara letu hili tulilopewa na Mungu. Viongozi wetu wa nchi za kiafrika inabidi wafanye mambo ya ziada ili kulinusuru bara hili na machafuko ya vita, ukame, ujinga, maradhi kwani mambo haya ndiyo yanayotufanya tujichukie na tulichukie bara letu, hivyo basi ili tuweze kuishi maisha mazuri tuweke mikakati itakayotuwezesha tufikie malengo yetu tunayoyakusudia, tuweke siasa pembeni na tuangaliye maslahi mapana ya kila mwafrika. Na kwanini ninazungumzia Afrika kwa ujumla, ni kwa kuwa ndiyo tuliyowengi wenye matatizo kwenye nchi zetu na ndiyo wengi wenye kukimbilia Ulaya, wazungu wanakaa mikutanoni kujadili wakimbizi wanaokwenda kwenye nchi zao, kwanini sisi waafrika wenyewe tusijadili kwanini ndugu zetu wanakimbia nchi zao?
Hivyo basi tuchangie mawazo ili tuone tunaanza wapi? na tufanye nini? kwa muda gani?
Ili nasi tuweze kuishi katika maisha ya ndoto zetu na tuwe kimbilio kwa wenye matatizo katika mabara mengine.
 
Ningekuomba uongelea nchi yetu Tz ....Africa ni kumbwa namatatizo tofouti tofouti, kuna nchi kama Tunisia Morroco, South Africa Egypt, Algeria, Botswana,Nigeria Seychelles, Libya, ziko vizuri ata kuliko baadhi ya nchi Ulaya na Asia huwezi kuzijumlisha na nchi kama Tz, Burundi, Mali, DRC, Bokina faso nk. hizo nchi hazina nyuma au mbele kila sector niya hovyo sana ndiyo zenye masikini ulio kithiri,kwamfano Tz inaongoza kwa natural resources ukitoa SA.........nchi kama Kenya, Ghana, Rwanda, Uganda, Ivory coast nk zinakosa vitu vidogo katika uongozi. Ku take off kwenye uchumi wakati.
 
Naona hii ndio suluhu.
 
Ni ndoto kwa Africa kuendelea,kwa viongozi hawa wenye chuki na kuamini kila aliefanikiwa ni mwizi.Labda tutawaliwe tena miaka 100,maana tumeshindwa kujiongoza.China ni mkoloni mpya japo hana tija.
 
Ikiwa kwako kuna neema na kwa ndugu na jirani zako hakuna neema basi bado utakuwa na wakati mgumu kwani hodi hazitoisha, hivyo ukiweza kuwawezesha ndugu na jirani zako katika kuishi maisha ya neema wao na wewe mtakuwa wenye kufurahia hiyo neema.
 
Ikiwa kwako kuna neema na kwa ndugu na jirani zako hakuna neema basi bado utakuwa na wakati mgumu kwani hodi hazitoisha, hivyo ukiweza kuwawezesha ndugu na jirani zako katika kuishi maisha ya neema wao na wewe mtakuwa wenye kufurahia hiyo neema.
Nyerere alipoteza rasilimari zetu husaidia nchi jilani kama Botswana South Africa Angola nk. Zimesha tupita kiuchumi no democrasia, nk sasa hivi wa Tznia wanakimbilia huku hupata green pasture " so to fight vya kwetu.
 
Nyerere alipoteza rasilimari zetu husaidia nchi jilani kama Botswana South Africa Angola nk. Zimesha tupita kiuchumi no democrasia, nk sasa hivi wa Tznia wanakimbilia huku hupata green pasture " so to fight vya kwetu.
Ni kweli wakati wa Nyerere viongozi wa kiafrika walikuwa wakisaidiana, lakini wakati ule tatizo kubwa ni kujikomboa kutoka kwa wakoloni na kweli tuliweza kupigania uhuru wetu. Na sasa tusaidiane kwa pamoja katika vita hivi vya kiuchumi kama bara la Afrika ambalo matatizo yake yanafanana kwa kuwa wengi wa wananchi wake wanaishi kwenye umasikini, na Nyerere alikuwa na ndoto kwenye mstari wa mbele kuhakikisha waafrika wananeemeka katika nchi zao, Charles de Gaulle alisema "The leader must aim high, see big, judge widely, thus setting himself apart form the ordinary people who debate in narrow confines." Na kwa msemo huu ni hakika kuwa Nyerere alikuwa kiongozi si kwa watanzania tu bali kwa waafrika kwa ujumla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…