GE2025 Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Katavi vyashiriki mazoezi ya pamoja

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA MKOA WA KATAVI VYASHIRIKI MAZOEZI YA PAMOJA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama Oktoba 3, 20205 wamefanya mazoezi ya matembezi (Route Match) kwa kutembea zaidi ya kilomita 10 kuzunguka maeneo mbalimbali Manispaa ya Mpanda.

Mazoezi hayo yamejumuisha Jeshi la Polisi, Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji na Idara ya Usalama.

Soma pia: Golugwa: Vyombo vya ulinzi na usalama visiwashambulie raia



Lengo la matembezi hayo ni kuimarisha mshikamano baina ya vyombo vya ulinzi na usalama, kujenga afya ya mwili na akili na kuendelea kujiweka tayari katika kulinda amani na usalama wa raia na mali zao.

Akizungumza baada ya mazoezi hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani amewapongeza washiriki wote na kuhimiza kuendeleza mshikamano katika kuhakikisha ulinzi na usalama unaendelea kuimarika.
 
Wakaribishwe kushiriki pia tarehe 29 oct.
 
Wananchi wangeunga hapo nyuma yao ili mazoezi yanoge
 
Hapo pichani wengi wao mishahara yao ipo chini ya 1M na wengi wao hawana vyeti walau form 4.

Hao ndio kizingiti kikuu cha mabadiliko
 
Natarajia kwa uovu wanaotwkeleza na waliotekeleza nisikie siku wana shiriki zoezi na kuuana wenyewe kwa wenyewe kwani wameshalevyiwa na damu zisizona hatia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…