Vyombo vya kutengea vyakula

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2015
Posts
28,448
Reaction score
44,622
Kuna vyombo vya kulia vyakula vyenye hadhi na visivyo na hadhi. Nadhani mna makabati ya kuwekea vyombo. Sio kila chombo kinastahili kuonekana kabatini, vinavyonekana ni vile vyenye hadhi tu. Kisaikolojia kuna watu ukiwatengea chakula kwenye vyombo vyenye hadhi utaonekana ni muungwana na una heshima na ukiwatengea kwenye vyombo visivyo na hadhi utaonekana huna busara, ni mkorofi na huna heshima, kama ni mmeo unamtengea hivyo unaweza kuzabwa makofi na vyombo hivyo kuvurumishwa mbali kama si kuvunjwa kabisa. Pika chakula na pakua kwenye vyombo vyenye hadhi usilete dharau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…