Wanadai wanatengeneza vyeti Uingereza, ambako kuna kampuni inayowatengenezea pia UDSM. Vyeti hivyo ati hutumia angalau miezi tisa kutengenezwa. Na mara nyingi muda huongezeka wafanyakazi wa vyuo husika wanapochelewa kupitia upya usahihi wa taarifa zilizomo ndani ya vyeti.
ni kweli vyeti vya UDSM,Muh2 nadhani na chuo cha ardhi hutengezwa nje kuepuka kuchakachuliwa manake vingetengezwa bongo kila mtu mtaani angejiita daktari.nakumbuka nlisubiri mwaka ndio nikapata cheti cha kuhitimu digrii ya kwanza.sii mbaya kwa vile wanalinda kuchakachuliwa na wabongo wajanga manake hata mwaziri walidiriki kujiita madaktari wkt phd hawana mfano nchimbi na Kamala,pia Lukuvi na hadi leo hawajathubutu kumfungulia mashtaka yule bwana aliewatangaza hadhanrani kwenye kitabu chake wamefoji elimu.
.....mie nilimaliza 2009 pia sijapata,ila vitakuwa vimetoka nadhani maana inaelekea miaka 2 sasa. Nina mpango wa kwenda kuulizia june maana hapo nitakuwa nakihitaji haswa ili nitafute ajira.
Hamna lolote la maana linalosababisha vyeti vichelewe kutoka zaidi ya urasimu uliokithiri kwenye vyuo vyetu.Siku hizi teknolojia ni kubwa hivyo haviwezi kuchelewa kama wana nia ya dhati.Mi nakumbuka tulichukua muda mrefu kupata hata academic transcript za MUCHS kisa eti gamba gumu la kuandikia hizo transcript lilikuwa limeisha! UCHENGE MTUPU!!!