Vyanzo cha fikra finyu za watanzania wengi

Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
6,673
22,339
Kwanza nawasalimu wanajamii kwa kuwa hii ni thread yangu ya kwanza toka nijiunge humu ...

Kwa miaka mingi nimekuwa nikijiuliza kuhusu suala la fikra finyu za watanzania walio wengi ambazo hudhihirishwa hasa na haiba zao. Baada ya kuchangamana na watu sana ,nilikuja kutambua vyanzo vifuatavyo vya hali hii :-

1. Makuzi katika jamii
Watoto wengi wa kitanzania hukuzwa katika imani za kutokujiamini katika kufanya mambo makubwa na pia hunyimwa haki yao ya kutoa mawazo katika familia na hivyo hushindwa kuiendeleza ari ya fikra pevu na udadisi .

2. Mfumo mbovu wa elimu
Elimu yetu haimuandai mtoto katika kuifungua akili yake na kuutambua uwezo wake zaidi kwa sababu ni elimu ya makaratasi inayowalazimu watoto kuweka malengo katika kufaulu mitihani tu ili kupata kada zinazotoa ajira bila hata ya kuiakisi talanta yake na hivyo kuifunga akili yake katika makaratasi tu .

3. Sera ya Ujamaa
Hii ilitengeneza hali utegemezi kwa serikali na hivyo kuzifunga akili za watanzania katika kutafuta suluhisho la matatizo yaliyo ndani ya uwezo wao kwa kuwa hata sukari walipewa.. Tokeo la hali hii ni watu kudai haki bila kutimiza wajibu wao na hivyo kuzidumaza fikra zao..

USHAURI WANGU:

1. Rais anapaswa kufanya maboresho katika mfumo wa elimu ili kumuwezesha msomi kuwa huru kifikra na pia kuiendeleza talanta yake. hili itafanikiwa kwa kuongeza bajeti ya elimu..

2. Mgawanyo wa madaraka kwa ngazi za chini za madaraka..hili litasaidia kuongeza nafasi ya watanzania katika kujiletea maendeleo yao wenyewe hivyo,kupunguza utegemezi kwa serikali kuu

**** TANZANIA KWANZA ****
 
Ninasikitika sana huu uzi mzuri haukuchangiwa.
Je uliwachoma watu?
 
** TANZANIA KWANZA **
Wewe vipi akili unazo

USSR
 
Huu uzi sikubahatika kuuona kwa kweli, wenye mamliaka wausome na kuufanyia kazi
 
Back
Top Bottom