shiddi
Member
- Jun 12, 2016
- 16
- 13
Salamu ndo jambo la kwanza,
Narudia tena kwenye siasa ili chama chochote kiweze kuwa imara sharti kiwe na vijana wazalendo na watu wenye moyo wa kufa na kupona kulinda na kukitumikia chama chao na kutekeleza ilani ya chama chao kwa moyo mmoja.
Tusitegemea kuwa wapinzani wenye nguvu kwa kutegemea wale walioachika kutoka kwenye vyama vingine. Andaa vijana wako hao ndo watakuwa na nguvu na uchungu. Vinginevyo mtaishia kuwa mnalalamika mara huyu ni msaliti mara ooh anatumiwa na chama fulani, mnasahau kuwa kama hicho chama kilimlea kikamsomesha mwisho wa siku akahama bado chembechembe itaendelea kuwamo moyoni mwake.
Kwa hiyo ushauri wangu vyama vya upinzani wekezeni nguvu nyingi kwa vijana maana wao nguvu yenu katika siku za usoni na tujenge utamaduni wa kuwaamini.