Vyama vya upinzani Afrika viunganishe nguvu zao

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,997
20,329
Vyama vya upinzani Afrika viunganishe nguvu zao kwanza ili kuondoa vyama vilivyokuwa vya ukombozi vilivyogeuka kuwa mkoloni,

Vifanye hivyo kabla yakusaka misaada toka Ulaya. Makoloni na mabeberu haya ya ndani ambayo zamani vilikuwa vyama vya ukombozi viliungana vikashinda enzi hizo...

Mfano kulikuwa na mashirikiano makubwa kati ya TANU na KANU ambapo makamanda na makomred walikuwa wakiazima ujuzi na mapambano katika uwanja wa vita.

TANU chini ya rais wake Julius Nyerere iliwahi kuwatuma Bibi Titi Mohame na Mzee Tambaza kwenda Kenya kuwasaidia KANU iliyokuwa chini ya Kenyatta na Tom Mboya.

Mpaka leo wakolo hawa washirikiana, yanayotokea Rwanda,Burundi,Kenya na Afrika kwa ujumla yote yana baraka za Tanzania. Yani haiumizwi
 
Vyama vya ukombozi vilikuwa vinapambana kukomboa mataifa na siyo kuwakomboa watu binafsi au kujinufaisha kibinafsi.

Vyama vya upinzani vya sasa kwa kiwango kikubwa ni watafuta fursa za kujinufaisha binafsi.

Mfano hai ni ujio wa Lowassa ndani ya CHADEMA na yaliyokuwa yanasemwa na wapinzani kabla Lowassa hajajiunga CHADEMA.

Kama wanashindwa kusimama kwenye maneno yao, unadhani wataweza kusimama kwenye malengo makuu.

Hata wewe ni wale wale tu ambao wanachokiandika siyo kile wanachokiamini.
 
Back
Top Bottom