Vyama vya siasa viwe viwanda vya kuzalisha viongozi bora

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
30,988
72,186
Sote twafahamu swala la uongozi ni nyeti kiasi gani...
kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi ni kwaajili ya kuchochea maendeleo,ushindani,kuibua madhaifu n.k.

"daktari hawi daktari pasipo kuusomea udaktari"lkn si kuusomea tu bali ahakikiwe kuwa amefuzu vyema pasi utata.. ningependa kauli hii pia iwe ktk vyama vya siasa kwamba "kiongozi hawi kiongozi pasipo kusomea uongozi kiuhakika na kuthibitika kuwa amefuzu vyema"
Hii itasaidia sana kuwa na product ya viongozi bora wenye upeo wa kile wanachokifanya.
si hivyo tu,bali kutakuwa na ushindani ulioshiba baina ya vyama vyote vya kisiasa bila kusahau na katiba isiyo naupendeleo.

kiongozi ni lazima afahamike itikadi zake,historia yake,machukulio yake na namna alivyo halafu alinganishwe na nini kinatakiwa ktk nchi.
Ni aibu kwa chama chochote kile kutokuwa na product nzuri ya viongozi wenye weledi wakujua nini wanafanya,kwanini wanafanya,na matokeo yapi yatapatikana baada ya kufanya... lzm tuwe na viongozi ambao ni deep thinker na watakaoleta maendeleo ktk nchi.
 
Back
Top Bottom