Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Ningependa kujua kuwa msanii ama wasanii na kuwa mfuasi wa chama cha siasa ni kinga ya kutoshitakiwa kwa kosa lolote ? Nimefuatilia kwa makini suala Wema Sepetu kuhama toka CCM kwenda Chadema nimeona halina mshiko wowote. Chadema wangesubiri mpaka hatima ya kesi ya Wema Sepetu ndio wangeamua ajiunge na chama hicho, Chadema isigeuke kuwa,kokoro kama ilivyokuwa CCM umaarufu wowote wa chama chochote cha siasa ni jinsi itakavyo wakomboa watanzania kutoka kwa hali walionao lakini sio kwa kutafuta sura za wasanii.
Ni wakati muafaka wa vyama vya upinzani kujijenga kisiasa badala kukimbilia kuwatetea na kuwapokea watuhumiwa wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali. Ni aibu kwa nchi kama Tanzania kushikwa mateka kisiasa na wasanii kama Wema Sepetu na Steve Nyerere.