Vyama vitano kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Vyama vitano vya siasa vitashiriki katika uchaguzi wa marudio wa Zanzibar, utakaofanyika Machi 20 mwaka huu, uliotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Vyama hivyo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), ADC, CCK, TLP na SAU.

Hatua hiyo inatokana na vyama vitatu vya siasa Zanzibar vya CCK, SAU na TLP, kutangaza kuwa wagombea wake, watashiriki katika uchaguzi huo wa Machi 20. Taarifa ya viongozi wa vyama vya CCK, SAU na TLP, iliyosomwa kwa pamoja katika Ukumbi wa Culture eneo la Mji Mkongwe jana, ilisema wagombea wa vyama hivyo vitatu, watashiriki uchaguzi huo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, ulifutwa baada ya kujitokeza kwa kasoro mbalimbali, zilizoonesha wazi kwamba hauwezi tena kuwa huru na haki.

Wagombea wa vyama hivyo vya siasa, waliotangaza kushiriki katika uchaguzi huo ni Ali Khatib kutoka CCK, Issa Mohamed Zonga kutoka SAU na Hafidh Hassan Simai kutoka TLP.

Mgombea wa CCK, Ali Khatib Ali alisema kwamba tayari wamejipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi huo na kuwataka wanachama na wafuasi wake na wananchi, kuitumia fursa hiyo ya kidemokrasia kuchagua viongozi watakaoongoza nchi.

“Tangazo la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) limetutaka kurudia uchaguzi kwa sababu ule wa awali umefutwa kwa hivyo hatuna sababu ya kususia uchaguzi huo na tunachofanya kwa sasa ni kuwataka wanachama wetu na wafuasi kujitayarisha kwa uchaguzi wa marudio,” alisema Ali.

Jumapili iliyopita, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alisema chama hicho kipo tayari kwa uchaguzi wa marudio Machi 20 kwa lengo la kuhakikisha kinashika dola.

Akihutubia mamia ya wanachama wao katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui wakati wa kuzindua maadhimisho ya miaka 39 ya CCM, Dk Shein alisema maamuzi ya kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu, yamefanywa na ZEC ambayo ndiyo chombo halali kwa mujibu wa Katiba cha kushughulikia masuala yote ya uchaguzi nchini.

Aliwataka wanachama na wafuasi wao kujipanga vizuri na kushiriki uchaguzi huo kikamilifu, kwani kwa mujibu wa Katiba ya CCM ni kushinda chaguzi zote zinazofanyika nchini ili kushika dola na kuwatumikia wananchi.

“Hayo ndiyo maamuzi ya chama chetu tuliyokubaliana kushiriki Uchaguzi Mkuu wa marudio baada ya kufutwa kwa ule wa Oktoba 25 mwaka jana kwa hivyo wanachama na wafuasi jitayarisheni kushiriki kikamilifu kwa ajili ya kushika dola,” alisema Dk Shein.
 
Zanzbar Inahitaji Maombi !
Lakini inahitaji Ukweli zaidi !!

Kuna watu wanapotosha kuhusu Uchaguzi wa Zanzibar wakidai ni wa marudio !

Ukweli ni kwamba ni Uchaguzi mpya unohitaji
Kuanza Upya Na wagombea waombe upya!!

Sifa za Uchaguzi wa Marudio kwa mujibu wa sheria duniani kote:

Kwanza :
Uchaguzi wa marudio
ni
ule ulioharibika kwenye
baadhi
ya maeneo ,Na hurudia maeneo husika .

Pili :
Uchaguzi wa Marudio ni ule ambao unaoongozwa

Na Sheria inayomtaka mshindi
kupata asilimia ya kura zaidi nusu ya waliopiga kura ,

Sifa za Uchaguzi uliofutwa :

1:Uchaguzi uliofutwa ni zaidi ya kuharibika''

2:Ni kama hakuna kilichokuwa kinafanyika

3heria zilikiukwa
kuanzia Uteuzi wa wagombea ,,,'

4:Wapiga kura walio wengi
hawakuwa Na sifa za kupiga kura

5:Upigaji kura haukukamilika katika maeneo yaliyo
Mengi !

6:Ni vigumu kuyatambua Na kuhakiki matokeo yaliyotoka vituoni. Nk

7:Ni kitu cha kuanza Upya kila hatua ikiwemo uteuzi wa wagombea

Kwa Maoni yangu :

Hii Tabia ya kurudia Mtihani
darasa zima, Kisa Mtoto wa
mwaalimu kafeli !!

Ikiendekezwa itatupeleka Tanzania pabaya !

Mwana wa Adili :
Kiwaryalema
 
CUF watakuja kushituka baada ya serikali ya umoja wa kitaifa kuundwa kwa kushirikisha vyama vilivyoshiriki uchaguzi wa marudio
 
Back
Top Bottom