Huwezi kushangilia mchezaji kumfanyia faulo mchezaji mwingine, hatukatai ni kweli kuna faulo za kiuanamichezo lakini si faulo za kukusudia kumuumiza mwenzako tena kwenye sehemu za mwili ambazo ni sensitive na zinaweza kusababisha kifo au mchezaji kupooza. Hivi ikitokea mchezaji kapooza au kufa kwa sababu ulimgonga kwenye spinal cord au kwenye medulla oblongata na team yako ikashinda au ikachukua kombe huo ushindi au hilo kombe litakuwa na thamani gani kwako huku kila mara unakumbuka kwamba ulisababisha mchezaji mwenzako kupooza au kufa?