Vodacom walifikia hatua ya kuridhika sana na wateja, kila mara wamekuwa wakipandisha bei. Najiuliza hivi hawa TCRA wanafanya kazi gani kama bei ya hii mitandao iko juu namna hii? Au kuna watu wana hisa huko ndio maana wanafanya wanavyotaka? Au bei zinapangiwa kampuni za umma tu kama TANESCO, mamlaka za maji na nyingine?
Na kama running cost ni kubwa, bei ya internet ya TTCL ni ndogo sana kuliko hawa. Tuliambiwa kuwa kuna mkongo wa taifa utakaopunguza gharama za internet na mawasiliano kwa ujumla. Lakini badala ya gharama kupungua ndio akina Voda na wenzake wanazidi kupandisha. Na kwa utafiti wangu ni kuwa, kila Vodacom akipandisha basi utaona na Tigo naye anapandisha.
Hata mimi nimefikia kuichukia kabisa Vodacom.